TEHRAN:Iran yasema Ng'o haibadili msimamo
4 Oktoba 2006Matangazo
Naibu mpatanishi katika mazungumzo yanayohusu mgogoro wa Nuklia wa Iran Abdolreza Rahmani Fazli amesema nchi yake haitokubali kuachana na mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.
Matamshi ya bwana Rahman yanakuja baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice na maafisa wengine wa nchi za Magharibi,kuonya kwamba Iran italazimishwa kufika mbele ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa endapo haitojitolea yenyewe kuachana na mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium.