TARO ASO.
24 Februari 2009Matangazo
WASHINGTON.
Waziri Mkuu wa Japan Taro Aso amewasili Washington kuwa kiongozi wa kwanza kutoka nje atakaekutana na rais Barack Obama katika Ikulu ya Marekani.
Waziri mkuu Aso anaefanya ziara ya siku moja nchini Marekani anatarajiwa kukutana na rais Obama leo.
Viongozi hao wanatazamiwa kujadili njia za kukabiliana na mgogoro wa fedha ulioikumba dunia.
AFP.