1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mchezo wa riadha watumbukia katika mgogoro

7 Novemba 2015

Mchezo wa riadha umetumbukia kabisa katika mgogoro huku Shirikisho la Riadha Ulimwenguni – IAAF likifuta tamasha lake la mwisho wa mwaka la kuwatuza wanariadha bora

https://p.dw.com/p/1H1Yi
Jamaika Läufer Usain Bolt IAAF Preis Lamine Diack Prinz Albert von Monaco
Picha: Getty Images/V.Hache

Hii ni baada ya maafisa wa Ufaransa kuanzisha uchunguzi dhidi ya rais wa zamani wa shirikisho hilo Lamine Diack kuhusu tuhuma za rushwa.

IAAF imetangaza kuwa imewafungulia mashtaka maafisa wanne wa riadha ya ukiukaji maadili kwa kuficha matokeo ya vipimo vya utumiaji dawa zilizopigwa marufuku michezono vya mwanariadha mmoja wa Urusi

Maafisa hao wanne, ni mshauri wa zamani wa IAAF Papa Massata Diack, mwanawe rais wa zamani Lamine Diack, rais wa zamani wa shirikisho la riadha la Urusi Valentin Balakhnichev, kocha wa zamani wa Urusi katika mbio ndefu Alexei Melnikov na mkurugenzi wa zamani wa idara ya kupambana na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu mwilini ya IAAF Gabrielle Dolle.

Rais wa IAAF Sebastian Coe amesema tamasha hilo lililopangwa Novemba 28 mjini Monaco ambalo huwatunza wanariadha bora wa mwaka halitaendelea kwa sababu ya kashfa ya utumiaji dawa za kuongeza nguvu mwilini inayolikumba shirikisho hilo. Hata hivyo amesema washindi wa tuzo za mwaka huu watatangazwa kwenye tovuti ya IAAF.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: