Taasisi ya CDC- Afrika yasema mataifa yasiokuwa na aina ya virusi vya Afrika Kusini yatumie chanjo ya AstraZeneca | Matukio ya Afrika | DW | 11.02.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Taasisi ya CDC- Afrika yasema mataifa yasiokuwa na aina ya virusi vya Afrika Kusini yatumie chanjo ya AstraZeneca

Taasisi ya Afrika ya kupambana na magonjwa- CDC- imesema nchi za Afrika ambazo hazijagundua maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha corona kilichozuka nchini Afrika Kusini zinaweza kuendelea na chanjo ya AstraZeneca.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo John Nkengasong ameuambia mkutano na waandishi habari kuwa kwa mataifa yaliyoripoti aina hiyo ya virusi zinapaswa kujitayarisha kutumia chanjo nyingine zote zilizoidhinishwa kupambana na COVID-19.

Kenya tayari imekwishasema kuwa itaendelea na mipango ya kutumia chanjo ya Astrazeneca na kupuuza wasiwasi wa ufanisi wa chanjo hiyo katika kutoa kinga dhidi ya viruis vya corona.

Afrika Kusini imesitisha kwa muda matumizi ya chanjo hiyo inayozalishwa na kampuni ya Astrazeneca na chuo kikuu cha Oxford baada ya taarifa za utafiti kuonesha inatoa kinga ndogo kwa aina mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa nchini humo.