1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yasisitiza mjadala wa kitaifa

21 Oktoba 2012

Mjumbe wa amani wa kimataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi Jumamosi (20.10.2012) amesisitiza mjini Damascus haja ya kusitisha mapigano, ili kuzuwia umwagikaji zaidi wa damu nchini nchini humo.

https://p.dw.com/p/16TxS
epa03439649 Syrian Foreign Minister Walid al-Moallem(R) meets with Lakhdar Brahimi, the joint UN-Arab League envoy, in Damascus, Syria, 20 October 2012. Brahimi flew in a day earlier to push for his plan to achieve a cease-fire during the four-day Eid al-Adha holiday that begins on 26 October. Brahimi has said he has no grand plan to end Syria_s civil war. Instead, he presented the truce as a 'microscopic' step that would alleviate Syrian sorrow temporarily and provide the basis for a longer truce. EPA/YOUSSEF BADAWI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria Walid al-Muallim akizungumza na Lakhdar BrahimiPicha: picture-alliance/dpa

Brahimi alikutana na waziri wa mambo ya kigeni Walid Muallem pamoja na viongozi wa upinzani wanaokubalika na rais Bashar al-Assad , katika juhudi za kupata kuungwa mkono mpango wake wa kupatikana usitishaji wa mapigano , wakati wa sikukuu muhimu ya Kiislamu wiki ijayo.

Lakini mazungumzo hayo yaligubikwa na hali ya wasi wasi katika nchi jirani ya Lebanon , ambako viongozi wa upinzani pamoja na waziri mkuu walihusisha shambulio lililosababisha mauaji ya afisa wa ngazi ya juu wa upelelezi na utawala wa Syria .

UN Arab League deputy to Syria, Lakhdar Brahimi, speaks during a press conference after meeting Lebanese Prime Minister Najib Mikati, at the government palace, in Beirut, Lebanon, Wednesday, Oct. 17, 2012. Brahimi is in Beirut to meet with Lebanese officials. (Foto:Bilal Hussein/AP/dapd)
Mjumbe wa kimataifa Lakhdar BrahimiPicha: dapd

Nchini Syria kiasi watu 108 wameuwawa katika ghasia siku ya Jumamosi , 42 kati yao ni raia, limeripoti shirika la kuangalia haki za binadamu nchini humo, wakati mapigano yakiendelea katika maeneo ya kaskazini na kuzunguka mji wa Damascus.

Kusitisha mapigano

Wizara ya mambo ya kigeni imesema waziri Muallem amejadili pamoja na Brahimi, kile walichokiita "hatua ya kusitisha mapigano, ili kujitayarisha kwa mjadala wa dunia juu ya Syria, bila kuingiliwa na ushawishi wa mataifa ya nje".

"Mjadala wa aina hiyo ndio njia pekee ya kutoka katika mzozo huo", wizara hiyo imesema.

Muallem pia amelalamika kwa Brahimi juu ya mataifa ya eneo hilo ambayo Syria inayashutumu kwa kuwahifadhi, kuwapa silaha na kuwapa mafunzo waasi, akisema kuwa vitendo vyao vinaathiri ujumbe wa mjumbe huyo wa amani wa umoja wa mataifa ya mataifa ya Kiarabu, Arab League.

Uturuki na Saudia zalaumiwa

Syria imeilaumu mara kwa mara nchi jirani ya Uturuki pamoja na nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta ya Saudi Arabia na Qatar kwa kuunga mkono wapiganaji waasi.

Brahimi ana matumaini ya kupata usitishaji wa mapigano wakati wa sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Adha, inayoanza Oktoba 26, akiamini kuwa hiyo inaweza kusafisha njia ya hatua za muda mrefu za amani.

Hassan Abdel Azim kutoka taasisi ya uratibu wa kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasia nchini Syria , kundi la upinzani linalovumiliwa na utawala wa nchi hiyo , ameunga mkono pendekezo hilo la kusitisha mapigano.

epa02803006 Lawyer Hassan Abdel-Azim, the Secretary General of the Arab Socialist Union party and the spokesman for the National Democratic Gathering, a coalition of leftist opposition movements, speaks at a press conference held in Damascus, Syria 30 June 2011. The opposition lawyer said last week that a recent speech made by Syrian President Bashar Assad was 'insufficient and not reassuring.' EPA/Youssef Badawi +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kiongozi wa upinzani nchini Syria Hassan Abdel-AzimPicha: picture alliance/dpa

Usitishaji kama huo wa mapigano unaweza kusafisha njia kwa ajili ya hatua za kisiasa , iwapo utapanuliwa kujumuisha kuachiwa huru kwa wafungwa ambao wamekamatwa na utawala wa nchi hiyo pamoja na usambazaji wa msaada wa madawa kwa raia walioathirika, amesema. "Ghasia nchini Syria zimefikia katika kiwango cha kutisha ambacho kinatishia usalama na uhuru nchi hiyo", Abdel Azim ameongeza baada ya kukutana na Brahimi.

Nayo makundi ya upinzani

Ukichukua msimamo mkali zaidi , makundi ya upinzani ambayo yako nje ya nchi hiyo yanasema utawala wa Syria ni lazima uchukue hatua ya mwanzo na kusitisha mashambulio yake ya kila siku.

Brahimi anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Assad baadaye leo (21.10.2012) katika juhudi za ujumbe wake mjini Damascus kuleta amani.

Mjumbe huyo amefanya ziara katika mataifa kadha ambayo yana ushawishi katika mzozo huu wa Syria katika muda wa wiki moja iliyopita, ikiwa ni pamoja na ziara nchini Lebanon na Iran, na kuonya kuwa ghasia zinaweza kusambaa na kuliwasha moto katika eneo lote.

Mwandishi : Sekione Kitojo /afpe

Mhariri: Amina Abubakar