Sylvia Mwehozi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.04.2017
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu ya DW Kiswahili

Sylvia Mwehozi

Mfahamu Sylvia Mwehozi, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.

 1. Nchi ninayotokea: Tanzania
 2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2012
 3. Nilivyojiunga na DW: Nilijiunga na DW kwa miezi sita ya mafunzo (internship) kabla ya baadae kuendelea kuwepo.
 4. Kwanini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Sababu ya kutaka kufahamu mambo mengi, kusafiri na kufika maeneo kadhaa nchini mwangu na ulimwenguni ni mojawapo ya mambo yaliyonivutia zaidi.
 5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Mbali na kusoma elimu ya darasani, nadhani mwandishi wa kweli ni yule mwenye kiu ya kufuatilia masuala mbalimbali yanayoendelea katika jamii yake.
 6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Mwanzoni ilikuwa ni vigumu kueleweka ukisema wewe ni mwandishi wa habari kwasababu watu walisema“hawa ni paparazi tu, huenda anaturekodi huyu.“ Ilionekana kama ni kazi ya umbea. Lakini  kwangu haikuwa changamoto ilikuwa ni fursa.
 7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Niliwahi kwenda Mara nchini Tanzania kufanya makala ya uchunguzi kuhusu ukeketaji, nilifanya mahojiano ynagu kwa siri pasipo gundulika lakini baadae waliponigundua walianza kunitafuta, ilibidi nihame nilipokuwa nalala nyumba ya wageni na nikaenda nyumbani kwa rafiki yangu mwanaharakati sasa usiku naskia nje watu wananisaka kwanini nimeingia kijijini na kufanya mahojiano, ulikuwa ni usiku ulionigopesha, na sikuweza tena kulala kijijini hapo kwa hofu ya maisha yangu badala yake ilinipasa kukimbia.
 8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Wakati nilipotembelea Marekani 2014, nilitamani sana kufanya mahojiano na rais Barack Obama lakini sikufanikiwa. Ni mtu ambaye nilitamani kumhoji, huena siku moja nitakutana nae.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com