1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUingereza

Sunak: Tutafanikiwa kuwapeleka wahamiaji Rwanda

7 Desemba 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesisitiza kwamba mpango wa serikali yake wa kuwapeleka watu wanaozafuta hifadhi nchini Rwanda utakuwa na matokeo, wakati mpango huo ukitishia chama chake cha Conservative

https://p.dw.com/p/4ZtY0
Großbritannien | Sunak hat Tories nicht im Griff
Picha: Kin Cheung/AP/dpa/picture alliance

Serikali ya Sunak iliweka wazi hivi karibuni mpango wake wa kuwapaleka watu wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda hapo jana Jumatano, jambo ambalo limeugharimu utawala huo kwa waziri wake wa uhamiaji kujiuzulu akisema kuwa mpango huo haukuwa na matokeo mazuri.

Hili ni pigo kwa waziri Mkuu Sunak anapojaribu kuwazuia wabunge wa mrengo wa kulia wachama cha Conservativekuasi madai yao kwamba Uingereza inapaswa kuacha mikataba ya kimataifa ili kuipa kipaumbele sera yake ya uhamiaji.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye ofisi yake iliopo katika Mtaa wa Downing, Sunak amesema ikiwa serikali itaendelea kudharau sheria ya haki za binadamu, Rwanda itaachana na mpango huo na hawatokuwa na chaguo lingine la kuwapeleka wahamiaji wanaoingia nchini humo kinyume na sheria na hiyo si dhima ya kufanikisha mpango huo.

Soma pia:Sunak ataka uungwaji mkono kupeleka wahamiaji Rwanda

Aidha, mwanasiasa huyo ameendelea kushikilia msimamo wake juu ya mpango huo tata akisema kwamba hatoruhusu Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu kuzuia safari za ndege zinazowasafirisha wahamiaji haramu kuelekea Rwanda chini ya muswada mpya ambao unawasilishwa bungeni. 

"Sitoruhusu mahakama ya kigeni kuzuia ndege ikiwa mahakama yetu imeingilia kati matakwa ya bunge letu kuu," alisema sema Sunak

Aliongeza kwamba atafanya kila linalohitajika kuufanikisha mpango huu "leo sheria mpya zimeweka wazi kwamba uamuzi wa iwapo utafuata hatua za muda zilizotolewa na Mahakama ya Ulaya ni uamuzi wa mawaziri wa serikali ya Uingereza pekee." Alisisitiza mbele ya waandishi wa habari.

Mpango mbadala kufanikisha sera ya Uhamiaji Uingereza

Jaribio la awali la kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda liliingiliwa kati na maamuzi ya mahakama dhidi ya serikali ya Uingereza huku waziri Mkuu Sunak ambae kwa sasa anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka katika chama chake cha Conservative kutunga sera ambayo itadhibiti uhamiaji haramu katika taifa hilo linalojaribu kuuinua uchumi wake.

Kwa sasa Sunak atajaribu kufanikisha sheria hiyo kupitia bunge, lakini alisema hataifanya kuwa kura ya imani katika jaribio la kuongeza uungwaji mkono wa chama. Kutofanikiwa kwa kura ya imani kunaweza kugharimu uchaguzi wa kitaifa.

Duru ya kwanza ya kura kuhusu sheria hiyo inatarajiwa kufanyika bungeni Desemba 12.

Ujerumani: Rasimu ya kuwarudisha watu katika mataifa yao

Baadhi ya wabunge kutoka katika chama cha waziri mkuu huyo wanasema kwa mara ya kwanza tangu Sunak kuchukua mamlaka kuna uwezekano kukumbana na changamoto ya kiuongozi.

Soma pia:Uingereza yasema bado itajaribu kuwapeleka baadhi ya wahamiaji Rwanda

Hadi sasa ni mbunge mmoja wa Conservative ambae ameonesha kutokuwa na imani na sheria hiyo hadharani akisema kuna wenzake sita pia ambao wameonesha msimamo sawia faragha na kuongeza kwamba kujiuzulu kwa waziri wa uhamiaji huenda ni anguko la utawala wa Sunak.

Mpango wa kuwapeleka wasaka hifadhi nchini Rwanda umeendelea kupata upinzani mkali kutoka kwa vyama vya upinzani na mashirika ya kutetea haki za binadamu, huku Rwanda ikionya kwamba itajiondoa katika mpango huo iliousaini hivi karibuni iwapo Uingereza haitoheshimu sheria ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.