Suharto kuzikwa leo huko Java | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Suharto kuzikwa leo huko Java

Mazishi ya kitaifa yamepangwa kufanyika leo ya maiti ya rais wa zamani wa Indonesia, Suharto, aliyeongoza utawala wa kidikteta wa kijeshi kwa miongo mitatu.

Utawala huo ulioungwa mkono na Marekani uliwaangamiza maelfu ya wapinzani.

Mwili wa Suharto umeondolewa kutoka nyumbani kwake katikati mwa mji mkuu Jakarta na kusafirishwa kwa ndege hadi makaburi ya familia yake ya Astana Giribangun katikati mwa Java.

Suharto alilazwa katika hospitali ya Pertamina mjini Jakarta kwa siku 23 lakini akafariki dunia jana baada ya baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi.

Raia wengi wa Indonesia, akiwemo rais wa zamani, Abdurrahman Wahid, wamesema kifo cha Suharto ni hasara kubwa kwa Indonesia.

Rais wa sasa wa Indonesia, Susilo Bambang Yudhyono, amewata waindonesia wote waimboee roho ya marehemu Suharto na kutangaza siku saba za maembolezi ya kitaifa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametuma risala ya rambirambi kwa serikali na wananchi wa Indonesia kwa kumpoteza kiongozi aliyeitawala nchi hiyo wakati wa kipindi muhimu katika historia ya Indonesia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com