1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Suharto azikwa kwao Indonesia

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cyi1

JAKARTA:

Kiongozi wa zamani wa Indonesia-Suharto, amezikwa rasmi kwa heshima za kijeshi.Rais Susilo Bambang Yudhoyono aliongoza sherehe za mazishi katika makaburi ya familia ya Suharto yaliyofanyika katika mji wa nyumbani kwa marehemu wa Solo Java.Suharto alifariki dunia jana jumapili baada ya baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi. Amekuwa hospitalini kwa kipindi cha zaidi ya wiki tatu mjini Jakarta.Mamia kwa maelefu ya waombolezaji walijipanga barabarani katika mji wa Solo,kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wao wa zamani, wakati maiti yake ilipokuwa inapelekwa kuzikwa.Kiongozi huyo wa zamani anasifika kwa kufanikisha uchumi wa nchi hiyo.Hata hivyo atakumbukwa kwa utawala uliokuwa na umwagikaji mwingi wa damu, visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na rushwa.