1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan zakubaliana utekelezaji wa makubaliano

6 Januari 2013

Marais wa Sudan na Sudan kusini wamekubaliana jana Jumamosi (05.01.2013)kuhusu muda utakaopangwa kwa ajili ya utekelezaji wa masuala muhimu,wakati walipokutana kwa faragha katika mji mkuu wa Ethiopia ,Addis Ababa.

https://p.dw.com/p/17Ejb
KHARTOUM, SUDAN: Leader of the Sudan People's Liberation Movement (SPLM), Salva Kiir (L), holds hands with Sudanese President Omar al-Bashir (C) and second Vice President Ali Osman Taha at a low-key ceremony in Khartoum 11 August 2005, during which Kiir was sworn in as Sudan's first vice president after the death of his predecessor John Garang. Kiir, 54, pledged to follow his legacy and work for peace and unity in the war-ravaged country. He took office less than two weeks after Garang was killed in a helicopter crash that raised fears for the future of a peace deal that ended 21 years of war between southern rebels and the government in Khartoum. EDS NOTE: Removing extraneous sentence. AFP PHOTO/KHALED DESOUKI (Photo credit should read KHALED DESOUKI/AFP/Getty Images)
Omar al-Baschir wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan kusiniPicha: KHALED DESOUKI/AFP/Getty Images

Usalama, mafuta na mipaka ni miongoni mwa masuala ambayo rais wa Sudan ya kusini Salva Kiir na mwenzake wa Sudan Omar Hassan al - Bashir waliyajadili mjini Addis Ababa kwa upatanishi wa umoja wa Afrika.

Pande hizo mbili zimekubaliana kuwa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika katika mwezi wa septemba mwaka jana yanapaswa kutekelezwa, bila masharti yoyote, amesema mpatanishi wa umoja wa Afrika , rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki. "Jopo letu linatayarisha utaratibu wa utekelezaji wa makubaliano yote yaliyokwisha fikiwa kwa kupanga muda maalum, amesema Mbeki.

South Sudan's President Salva Kiir (L), Ethiopian Prime Minister Hailemariam Desalegn (C) and Thabo Mbeki (R), the chief mediator for talks between South Sudan and former civil foe Sudan, meet in Addis Ababa on January 4, 2013. Kiir is in the Ethiopian capital on Hailemariam?s invitation to meet with his Sudanese counterpart, Omar al Bashir, to push for progress on stalled oil, border and security talks. The two former civil war foes signed a raft of agreements in September, but none have yet been implemented, with the South accusing Khartoum of fresh attacks this week. Negotiations between the two rivals have been ongoing since Juba split from the North in July 2012, and though a series of deals have been forged, none have been successfully put in place. AFP PHOTO/JENNY VAUGHAN. (Photo credit should read JENNY VAUGHAN/AFP/Getty Images)
Rais wa Sudan kusini katika mazungumzo na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na mpatanishi Tambo MbekiPicha: Jenny Vaughan/AFP/Getty Images

Muda utakaopangwa utakamilika ifikapo Januari 13, Mbeki amesema. " Mkutano huo unapaswa kuhakikisha kuwa maamuzi muhimu yanachukuliwa ili kuunda eneo salama ambalo halitakuwa na shughuli za kijeshi," kama ilivyoelezwa katika mkutano wa Septemba.

Makubaliano ya awali

Pande zinazohusika zilikubaliana kuweka maeneo hayo katika mpaka wao wenye urefu wa kilometa 2,000 ambalo limekubalika. Hakuna makubaliano ambayo yamefikiwa kuhusiana na mpaka wa karibu kilometa 500, na pia katika jimbo la Abyei ambalo linadaiwa na kila upande kuwa ni lake.

** FILE ** In this Sept. 14, 2008 file photo, South African President Thabo Mbeki speaks at a press briefing in Pretoria, South Africa. South Africa's ruling party on Saturday, Sept. 20, 2008, called on President Mbeki to resign as head of state. (AP Photo/Denis Farrell, File)
Rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo MbekiPicha: AP

Jimbo la Abyei liko katika mpaka wa Sudan na jirani yake upande wa kusini, nchi ambayo imepata uhuru wake Julai 2011. Eneo hilo lilikaliwa kwa muda na majeshi ya Sudan kusini mwezi wa Mei, baada ya jeshi la upande wa Sudan ya kaskazini kuondoka kufuatia kulikalia jimbo hilo kwa muda wa mwaka mmoja.

Kamishna wa jimbo la Abyei, Rahma Abdel-Rahman al-Nour, ameliambia shirika la habari la dpa kuwa suala la Abyei linaweza tu kutatuliwa mara masuala ya kiusalama yatakapokubaliwa.

--- 2012_10_25_sudan_südsudan_abyei.psd
Ramani inayoonesha jimbo la Abyei

"Jimbo la Abyei limo ndani ya jimbo linalogombaniwa la Kordofan ya kusini; Iwapo jeshi la Sudan ya kusini halitaondolewa kutoka Abyei pamoja na maeneo mengine ya mpakani, Abyei itabakia kuwa katika hali tete," amesema al-Nour, ambaye yuko karibu na utawala wa chama cha rais al-Bashir cha National Congress.

Katika hatua nyingine , muungano wa vyama vya upinzani pamoja na makundi ya vyama vya kijamii umetia saini makubaliano siku ya Jumamosi (05.01.2013) mjini Khartoum ukitoa wito wa kuangushwa kwa utawala wa Sudan na kufanya uchaguzi huru na wa haki.

Makubaliano hayo , yaliyopewa jina la "Mapambazuko mapya, " yanalenga katika kuleta suluhisho kwa uchumi wa Sudan pamoja na mzozo wa kisiasa , elimu na afya.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Bruce Amani.