Sudan Kusini yaongoza kukiuka haki za binadamu | Matukio ya Afrika | DW | 29.04.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Sudan Kusini yaongoza kukiuka haki za binadamu

Serikali ya Sudan Kusini kwa sasa inatajwa kuongoza kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu,unaofanywa na viongozi wa chache wa serikali ya nchi hiyo na kukwamisha ujenzi wa taiafa hilo,kiuchumi na kijamii

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit

Mkurugenzi mtendaji Shirika la Ebony,taasisi ya isokuwa ya kibaishara mjini Juba Sudan Kusini,Lual Deng amesema kwa hali ilivyo sasa,nchi ya Sudan Kusini inaelekea ipo kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Somalia,na kama juhudi za haraka hazitachukuliwa,itakuwa kama moja ya nchi hizo kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Lual Deng ameyaeleza hayo wakati wa mjadala wa namna ya kuiinuna Sudan Kusini baada ya utawala wa nchi hiyo kuendelea kuwa katika mikono ya watu wachache na ufisadi kushika kasi,hasa baada ya Dola bilioni 8 za pato la mafuta la mwaka uliopita kuibiwa na maafisa wa serikali ya nchi hiyo.

Kufatia hali hiyo,wataalamu na wasomi mbalimbali nchini humo wameitaka Marekani na jamii ya kimataifa kuongeza shinikizo kwa serikali ya Sudan Kusini ili kuzungumzia udhaifu uliopo katika serikali kuu ya nchi hiyo, ikiwa ni kufuatia ripoti ya Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani.

Ufisadi unatishia Sudan Kusini

Majeshi ya Sudan Kusini

Majeshi ya Sudan Kusini

Vitendo vya ufisadi na serikali kushikwa na watu fulani,vimeripotiwa katika ripoti ya haki za binadamu iliotolewa na Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani katika ripoti yake ya mwaka,kuhusu haki za binadamu ulimwenguni.

Ripo hiyo imeonesha namna serikali ya Sudan kusini ilivyohusika katika kukiuka haki za binadamu kwa mwaka uliopita,ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kupa uhuru wake kutoka Sudan,baada ya vita kati yake na Sudan ambayo inatajwa kuchangia sana katika kukiuka haki za binadamu katika miaka ya ya hivi karibuni.

Serikali ya Sudan Kusini inadaiwa kufanya maovu kwa kutumia vibya vyombo vya usalama,kutokuwepo na uadilifu na kuendelea mapigano nchini humo,yote hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kukiuka haki za binadamu.

Mbali na hilo ripoti hiyo ya wizara ya nje ya Marekani imeonesha kuwapo kwa hukumu za vifo zinatotekelezwa na mahakama nchini humo,mateso,ubakaji na rushwa katika mahakama,kuwahamisha raia katika makazi yao na kuendelea mapaigano kati ya majeshi ya Sudan Kusini na Sudan.

Wanaharakati wa haki za binadamu wa mashirika kadhaa likiwemo shirika la Act for Sudan,wameitaja ripoti hiyo kama nafasi muhimu kwa Sudan kusini kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko hayo ili kuhakikisha maovu hayo hayatokei tena katika nchi hiyo.

''Lazima iwe wazi kuwa tunapoisaidia sudan Kusini kama zinavyofanya taasisi mbalimbali za kimataiafa,hatuna maana kuwa tunafumbia macho ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali hiyo,ati kwa sababu nchi hii ni mpya na inakabiliwa na changamo mbalimbali za ujenzi wa taiafa hilo ''Amesema John C.Brandishaw Mkurugenzi mtenfdaji wa shirika la The Enough Project wakati akizungumza na Shirika la habari la IPS.

Amesma kuwa ili kumaliza tatizo hilo,kuna haja ya kurudi nyuma na kuangalia historia ya Sudan Kusini kwa kuhamasishi wananchi wake waliotawanyika kurudi kushika nafasi muhimu ya madaraka ya nchi hiyo, na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit kukomesha rushwa na ufisadi katika nchi yake.

Kwa upande wake Muhadhiri wa chuo cha Smith Profesa Erik Reeves mtaalamu aliebobea katika masuala ya Sudan na Sudan Kusini amesema kutosomwa kikamilifu kwa ripoti yote kuhusu Sudan Kusini kunaweza kusababisha kutopata ufumbuzi wa tatizo la Serikali ya Sudan Kusini.

Ameikosoa ripoti hiyo kuhusu Sudan Kusini akisema ripoti hiyo imeisahau nchi jirani ya Sudan,ambayo ndio inachangia kwa kiasi kikubwa kutoa msaada kwa vikosi vya jeshi la nchi hiyo kuendelea kufanya mashambulizi dhidi ya Sudan Kusini.

Mwandishi:Hashim Gulana/IPS

Mhariri: Mohamed Abdulrahaman