Steinmeier-Georgia | Matukio ya Kisiasa | DW | 18.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Steinmeier-Georgia

Waziri wa nje wa Ujerumani apatanisha mzozo wa Georgia na Abchasia.

Mgogoro wa miaka kadhaa juu ya maeneo 2 yaliojitenga kutoka Georgia, sasa umezidi kupambamoto.Waziri wa nje wa nje wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeier,amefunga safari ya Georgia kujaribu kupatanisha.

Akiwa safarini kwa ndege kuelekea Tiflis, Bw.Steinmeier hakuweka ndoto kuwa itakua rahisi hivyo kufanikisha juhudi hii ya Ujerumani ya kuumaliza ugomvi huu wa Abchasia.

Ufumbuzi rahisi hautakuwapo.Hatahivyo, haitakua kuonesha dhamana kuwachia kutapakaa -alisisitiza kwa waandishi habari waliosafiri nae kuhusu dharura iliopo kuutuliza mzozo huu.

Mara tu baada ya kuwasili Tiflis, mji mkuu wa Georgia ili kukutana na wajumbe wa serikali na Upinzani,waziri wa nje wa Abchasia,eneo lililojitenga na Georgia, Schamba alibainisha wazi kabisa kuwa wao hawakusudii kujadiliana na Bw.Steinmeier juu ya hadhi za na malka ya Abchasia.Bw.Steinmeier anatarajiwa leo kuwasili Suchumi,mji mkuu wa Abchasia.

Eneo hilo lililojitenga na Georgia, halitambuliwi na mataiofa mengine ulimwenguni.hatahivyo, linagombea kuunda dola lake binafsi.Wakati Georgia inapinga kabisa kujitenga kwa eneo lake la Abchasia, Urusi inaungamkono Abchasia.

Mpango wa hatua 3 wa Ujerumani ili kuumaliza mgogoro huu, unajumuisha mbali na kujenga imani kati ya pande hizo mbili, pia hatua za misaada ya fedha ya kuijenga upya Abchasia na kurejea huko kwa wakimbizi robo-milioni wa Georgia.

Ni baada ya hatua hizo ndipo hadi na mamlaka ya Abchasia zifafanuliwe.Ujerumani ndio inayooongoza kikosi cha UM cha kuhifadhi amani kinachojumuisha pia askari wa Uingereza,Ufaransa,Urusi na Marekani.

Waziri wa nje wa urusi Sergej Lawrow, anakosoa mapendekezo ya ujerumani.Kwa hali ya sasa ni vigumu kabisa kufikiria kurejea kwa wakimbizi hao wa Georgia.Hali ya mambo yapasa kwanza kutulia.Iwapo mada hii itaingizwa katika ajenda ya mazungumzo ya kwanza ,basi mlango unafugwa kuingilia suluhisho lolote na pia azimio lililotungwa na Urusi kwa Umoja wa M ataifa.

Lawrow anasema:

"Tumelikabidhi Baraza la Usalama la UM azimio letu linalolenga kuutatua mzozo mkubwa uliopo-nao ni kutiwa saini mapatano kuwa kila upande unajizuwia kutumia nguvu.Hatari hii imeselelea na tunataka kukomesha uvumi wowote juu ya kuutatua mzozo huu kwa matumizi ya nguvu."

Alisema waziri wa nje wa Urusi Sergej Lawrow.

Wiki chache zilizopita, mabomu yakiripuka huko Abchasia na mapigano ya risasi katika Ossetia. Visa hivi vimechochea balaa la kuripuka vita vipya .Na kila upande umekuwa ukiutuhumu mwengine.

Waziri wa nje wa Ujerumani kwahivyo, katika mazungumzo yake leo huko Abchasia,hakabiliwi na kazi rahisi kusukuma mbele majadiliano baina ya pande 3-Georgia,Abchasia na Urusi.Akiwa mjini Tiflis, mji mkuu wa Georgia, alitoa mwito hapo jana kwa pande zote:ziachane kabisa na tabia ya kutumia nguvu .Kutozungumza na kuwekeana shuku si suluhisho la kuzipeleka pande zote mbele-alihimiza waziri wa nje wa Ujerumani Bw.Steinmeier.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com