Steinmeier ataka Ujerumani ijihusishe zaidi kupambana na mizozo | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.01.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Steinmeier ataka Ujerumani ijihusishe zaidi kupambana na mizozo

Ujerumani ni kubwa mno, kuweza kuzungumzia sera za dunia pekee, anasema waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier. Kuna umuhimu wa kuwa na msimamo maalum, licha ya kuwa dunia imebadilika.

Berlin Aussenminister Steinmeier im Bundestag 29.01.2014

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier

Hususan lakini wizara hiyo ya mambo ya kigeni ilipokuwa chini ya mtangulizi wake Guido Westerwelle ambapo ilipoteza uzito wake. Steinmeier anaona utamaduni wa kujiweka kando katika mizozo ya dunia, ambao Westerwelle aliukumbatia, kuwa ni makosa. Kwa hilo hayuko peke yake.

Hata waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen kutoka chama cha CDU amekuwa akitoa matamshi ya wazi katika siku zilizopita kuchukua hatua za kuzingatia hilo. Katika mauaji na matumizi ya nguvu Ujerumani haipaswi wakati huu kuwa mtazamaji tu, amesema waziri huyo akitilia maanani upelekaji wa vikosi vya jeshi la Ujerumani nchini Mali.

Msimamo

Mawaziri wawili katika nyadhifa hizo muhimu, ni lazima watoe msimamo thabiti. Von der Leyen anapaswa kama waziri wa ulinzi kuonyesha wazi mwelekeo wa wizara yake. Lakini ni lazima mwanasiasa huyo mkakamavu , kuzingatia, kwamba uongozi wake katika wizara hiyo sio kwamba haujawahi kutokea katika Ujerumani.

Ursula von der Leyen

Waziri wa ulinzi Ursula von der Leyen

Steinmeier anaweza hapa kuwa mtulivu. Hapo nyuma aliweza kuiongoza wizara hii vizuri. Lakini ndio sababu anapaswa kuonyesha ubora wake tena, kwamba yeye kama mwakilishi wa chama mshirika kinachounda serikali ya mseto sio kama mtangulizi wake kuwa ni njia ya kupitishia sauti ya kansela. Kwa hilo hata yeye anasababu za kutosha , kuweka msimamo wake.

Kilicho kipya hapa sio tu msimamo wake, hapa kuna mpaka ama kwa wastani kwa kile kinachoitwa nadharia za Merkel, kwamba Ujerumani haiwezi binafsi kupambana kijeshi, ama kupeleka silaha ama kwa njia nyingine kuwasaidia washirika wetu.

Upelekaji wa majeshi.

Ujerumani inajionesha , kwamba imeweza kuzuwia mbinyo wa kimataifa , kwa mfano kuhusu msimamo wake kuhusiana na upelekaji wa vikosi vya jeshi nchini Libya. Msimamo huu ulikuwa haujakuwa mzuri kuhusiana na maslahi ya Ujerumani katika kupata kiti cha kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Hazikuwa nzuri pia katika nchi , ambayo inachukua nafasi ya juu katika bara la Ulaya na katika uchumi wa taifa ambao ni muhimu duniani. Licha ya kuwa kuna sababu ya msingi kwa Ujerumani kujizuwia kutuma majeshi nje.

Kukataa matumizi ya nguvu kumepata mizizi imara hii leo katika jamii ya Wajerumani. Hii ni hali nzuri na haitabadilika katika wakati huu wa Steinmeier. Kwa hiyo waziri wa mambo ya kigeni haondoi moja kwa moja uwezekano wa kupeleka majeshi ya kupambana.

Steinmeier ni waziri sahihi wa kuchukua uamuzi, kwamba suluhisho la amani kila wakati ndio lengo sahihi, lakini pia upelekaji wa vikosi vya kupambana vya jeshi pia ni kitu cha kutiliwa maanani, kwa kuwa sera hiyo nayo ni mbinu ya kuweka mbinyo.

Mwandishi: Julia Bernstorf / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com