SPD yarejea madarakani jimboni NRW | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

SPD yarejea madarakani jimboni NRW

Uchaguzi muhimu katika mwaka huu 2012 hapa Ujerumani ,umefanyika katika jimbo la NorthRhine Westphalia.Wapiga kura wamelichagua bunge jipya la jimbo hilo Jumapili (13.05.2012) bila ya kubadilisha uongozi uliokuwapo.

Hannelore Kraft, federal state premier of North-Rhine Westphalia (NRW) and top candidate of the Social Democratic Party (SPD) stands next to her husband Udo and son Jan as she addresses supporters after first exit polls for the NRW federal state election in Duesseldorf May 13, 2012. Chancellor Angela Merkel's conservatives suffered a crushing defeat on Sunday in an election in Germany's most populous state, a result which could embolden the left opposition to step up its criticism of her European austerity policies. REUTERS/Wolfgang Rattay (GERMANY - Tags: POLITICS ELECTIONS)

Landtagswahlen in Nordrhein-Westfalen Hannelore Kraft jubelt in Duesseldorf auf der Wahlparty der SPD

Japokuwa matokeo hayo yalitarajiwa , lakini nchi nzima ilikuwa inakodolea macho kwa shauku kubwa uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na uongozi mzima wa serikali ya kansela wa Ujerumani. Hilo hata hivyo si jambo geni. Jimbo la North Rhine Westphalia lina wakaazi milioni 18 na jimbo hilo linachangia kiasi ya robo ya pato jumla la taifa, na uchaguzi wa jimbo hilo mara zote huchukuliwa kama uchaguzi mdogo wa bunge la taifa.

Pamoja na hayo katika uchaguzi wa mwaka 1966, 1995 na 2005 , vyama vinavyounda serikali katika jimbo hili , viliingia madarakani katika uchaguzi mkuu wa taifa. Uchaguzi wa jana hata hivyo uliangaliwa kwa shauku hadi dakika ya mwisho kuweza kufahamu iwapo ushindi wa chama cha SPD ungeweza kutosha kuunda serikali pamoja na chama cha kijaniUlikuwa uchaguzi mgumu, ambao uliwahusu zaidi watu, amesema Kraft.

ARCHIV - Sylvia Loehrmann, Spitzenkandidatin der Gruenen in NRW, posiert am 9. April 2010 in Duesseldorf, Nordrhein-Westfalen, waehrend des Wahlkampfauftaktes ihrer Partei fuer die Fotografen. Gruene ist sie mit Leib und Seele: Seit 25 Jahren gehoert Sylvia Loehrmann der Oeko-Partei an. Als Spitzenkandidatin bei der Landtagswahl in Nordrhein-Westafalen will die langjaehrige Fraktionsvorsitzende den Sprung in die Regierung schaffen. Eine Wiederauflage von Rot-Gruen schwebt ihr nach dem Machtverlust im Jahr 2005 vor, aber auch einem schwarz-gruenen Buendnis ist die 53-Jaehrige nicht abgeneigt. (apn Photo/Roberto Pfeil, Archin) ** zu unserem Portraet ** --- FILE - Green party top candidate Sylvia Loehrmann poses during the opening of the party's election campaign for the upcoming state election in North Rhine-Westfalia in Duesseldorf, Germany, in this April 9, 2010 file photo. (apn Photo/Roberto Pfeil, File)

Mgombea wa chama cha kijani Sylvia Löhrmann

Katika furaha hiyo ya ushindi chama cha kijani kimechanganya pia na hali ya kujisikia ahueni. Chama hicho kwa mara nyingine tena kimefanikiwa kufanyakazi pamoja na SPD.

Uchaguzi uliotishwa na mapema katika jimbo hilo , umekipa chama cha CDU matokeo mabaya kabisa kuwahi kutokea katika jimbo hilo, chama hicho kikiambulia kiasi ya zaidi ya asilimia 26 tu kwa mujibu wa matokeo ya awali jana.

Ikiwa imebakia miezi 16 kabla ya kuingia katika uchaguzi wa taifa na Merkel kuwania kipindi cha tatu cha uongozi , kansela anakabiliwa na kazi ngumu ya kutathmini ni vipi anaweza kuhakikisha ushindi kwa chama chake cha CDU pamoja na kuhakikisha sera zake za kupambana na mzozo wa madeni katika eneo la euro zinatekelezwa.

Bundesumweltminister Norbert Röttgen verfolgt am 15.11.2011 in Leipzig den CDU-Parteitag. Beim 24. Bundesparteitag der CDU beschäftigen sich die rund 1000 Delegierten vor allem mit den Themen Mindestlohn, Schulpolitik, Euro-Krise und Betreuungsgeld.. Foto: Bernd von Jutrczenka dpa

Mgombea wa chama cha CDU Nobert Röttgen

Afisa mwandamizi wa CDU hata hivyo amekana kuwa kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo kutaathiri sera za kitaifa za chama hicho. Lakini hali hiyo ya kushindwa vibaya imemlazimu mgombea wa chama cha CDU Norbert Röttgen kuachia ngazi ya uongozi wa CDU katika jimbo hilo. Norbert amesema:

"Ni wazi tumeshindwa, ni machungu na inauma sana. Matokeo haya yananilazimu , kukabidhi madaraka ya uongozi wa chama cha CDU katika jimbo hili."

Nacho chama cha FDP mshirika mkuu katika serikali ya mseto ya kansela Merkel kimepata mtu maarufu ambaye hadi mwaka 2011 alikuwa katibu mkuu wa chama hicho Christian Lindner. Amefanikiwa kukivusha chama hicho na kupata zaidi ya asilimia 5 ya kura na kufanikiwa kuingia katika bunge.

Chama kipya cha Pirates kinashangiria kwa mara nyingine tena , kimefanikiwa kuingia katika bunge katika jimbo la nne sasa.

Mwandishi: Scholz, Kay-Alexander/ ZR/Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com