Somlia-mamia wauwawa ? | Habari za Ulimwengu | DW | 30.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Somlia-mamia wauwawa ?

MOGADISHU:

Kamati ya Msalaba mwekundu ulimwenguni imearifu kwamba mamia ya watu yamkini wameuwawa katika mapigano ya hivi karibuni nchini Somalia na kuwa maalfu ya wengine wametimuliwa majumbani mwao na mapigano hayo.

Wakati shirika la wakimbizi la UM limeonya juu ya wimbi la wakimbizi wa kisomali kumiminika katika nchi jirani, chama cha msalaba mwekundu ulimwenguni kinadai hakuna wimbi kubwa hivyo la wakimbizi.

Chama cha msalaba mwekundi kinaarifu badala ya kukimbia, watu wanarejea maskani mwao mjini Mogadishu.

Jana, waziri-mkuu wa serikali ya mpito ya Somalia, Ali Mohamad Gedi,aliwasili Mogadishu akipongewa kwa shangwe.

Hii imekuja siku 1 tu baada ya vikosi vya serikali ya Somalia vikungwamkono na majeshi ya Ethiopia kuudhibiti tena mji mkuu Mogadishu-masaa tu baada ya wanamgambo wa Mahkama za kiislamu kuuhama mji huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com