1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soko la mitumba "Flohmarkt"

29 Agosti 2013

Katika nchi za Kiafrika ni kawaida kwa watu, hasa wasichana na wanawake kununua nguo katika masoko ya mitumba. Lakini hata hapa Ujerumani yapo masoko ya aina hiyo. Yanaitwa flohmarkt - ikimaanisha soko la chawa.

https://p.dw.com/p/19YRJ
Soko la mitumba "Flohmarkt"
Soko la mitumba "Flohmarkt"Picha: Elizabeth Shoo

Leo tupo katika soko moja la hapa mjini Köln. Ni soko linaloitwa Flohmarkt ambapo wanaouza hapa si watu wanaofanya shughuli hiyo kama kazi yao rasmi bali ni watu wa kawaida tu wanaokusanya vitu nyumbani kwao, vitu ambavyo hawavihitaji tena. kwa kawaida vitu hivyo huuzwa kwa bei rahisi. Mara nyingi utakuta nguo, viatu, pochi, vitu vya nyumbani kama vikombe, sahani na hata vitu vingine vya zamani. Wakati mwingine utapata hata vitabu vya zamani ambavyo havipo tena madukani ila ukija katika soko kama hili unaweza kuvipata. Nikiangalia hapa naona watu wengi wamekuja na meza zao, wameleta bidhaa zao na wamezitandaza na wanajaribu kuzinadi na kuvutia wateja ili waje kununua vitu kwao.