1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kupambana na dhuluma za kingono

Mitima Delachance19 Juni 2019

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, wahanga wa ubakaji toka maeneo tofauti wameandaa siku ya maonesho ya kazi mbalimbali wanazozifanya mjini Bukavu mashariki mwa nchi hiyo, ili kujaribu kusahau kilicho wapata. 

https://p.dw.com/p/3Kitp
Kongo Frauen sexueller Gewalt
Picha: Getty Images/T. Karumba

Juni 19, ni siku ya kimataifa  ya kupambana na dhuluma za kingono katika maeneo yanayokabiliwa na migogoro. Nchini jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wahanga wa ubakaji toka maeneo tofauti wameandaa siku ya maonesho ya kazi mbalimbali wanazozifanya mjini Bukavu mashariki mwa nchi hiyo, ili kujaribu kusahau kilicho wapata. 

Wengi wao wakiwa ni wanawake wenye umri kati ya miaka kumi na sita na sabini, wanawake hao wameonesha mabango, picha, maua, vitenge, vitunga, mapambo, na vyombo mbalimbali wanavyo tengeneza tangu pale walipopewa matibabu baada ya madhila waliyoyapitia ya ubakaji. Mkaazi mmoja wa eneo hilo Guillaumette Tsongo amesema lengo ni kuonesha kwamba baada ya mkasa huo, maisha yanaendelea kawaida Kivu Kaskazini.

Hata hivyo, wahanga wa ubakaji wanashuhudia kwamba bado wanazidi kukumbwa na unyanyapaa katika jamii kila leo, licha ya juhudi zote za uhamasishaji wa jamii kuaswa kutofanya hivyo. Wanaelezea kusikitishwa kwao hasa pale watoto wao walio zaa kutokana na ubakaji wanapo Baguliwa.

Tangu zaidi ya myaka kumi, jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inapambana na vitendo vya ujeuri na ubakaji dhidi ya wanawake. Majeshi ya nchi hii yanapambana na makundi yenye kumiliki silaha yanayo dhaniwa kuendesha ubakaji kwa kiasi kikubwa, na pia sheria ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imechunguza kesi nyingi za ubakaji na kutoa hukumu.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukiitambua siku hii tangu mwaka 2015.