Siku ya kimataifa ya Amani
21 Septemba 2012Matangazo
Huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanawake wameketi kutafakari masaibu wanayoyapata kutokana na kukosekana kwa amani katika eneo lao, na nchini Togo, maelfu ya wanawake wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo, wakitaka sauti zaidi katika maamuzi yanayohusu usalama wao. Kutaka kujua hali ya akina mama kiusalama kwenye siku ya leo, Daniel Gakuba mezungumza na Rukia Subow, mwenyekiti wa shirika la maendeleo ya akina mama nchini Kenya, na ameanza kwa kuzungumzia madhara ya vita kwa wanawake.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Daniel Gakuba
Mhariri:Miraji Othman