sherehe
12 Februari 2011Watu nchini Misri walisherehekea usiku kucha baada ya Rais Hosni Mubarak kujiuzulu.
Watu waliimbia, honi za magari zilipigwa, fataki ziliwashwa na watu walikusanyika kwenye uwanja wa ukombozi wa Tahrir mjini Kairo ili kufunga sala.
Baada ya kuitawala Misri kwa muda wa miaka 30 Rais Hosni Mubarak alijiuzulu hapo jana kufutia shinikizo kubwa la watu wake.
Maalfu kwa maalfu ya watu wamekuwa wanaandamana kwa wiki kadhaa kumtaka rais huyo aondoke madarakani.
Jeshi sasa limechukuwa mamlaka chini ya uongozi wa Mohammed Hussein Tantawi ambaye mpaka sasa bado ni waziri wa ulinzi.
Wakati huo huo mashirika ya habari yamearifu kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu Amr Mussa atajiuzulu wadhifa wake wiki zijazo. Bwana Mussa ambae hapo awali aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Misri anazingatiwa kuwa mtu mwenye uwezekano wa kuushika wadhifa wa Rais.