1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUgiriki

Serikali ya Ugiriki akabiliwa na kura ya kutokuwa na imani

28 Machi 2024

Serikali ya Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis inakabiliwa na kura ya imani bungeni hii leo, kufuatia ripoti za vyombo vya habari wiki hii vikidai kuchezea ushahidi.

https://p.dw.com/p/4eECK
Ugiriki |Waziri Mkuu Kyriakos Mitsotakis
Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis katika picha iliyopigwa Febrauri 15, 2024. Mitsotakis anakabiliwa na kitisho cha kuondolewa madaraka kwa shutuma za kudanganya kuhusu ajali ya terniPicha: Louisa Gouliamaki/REUTERS

Vyama vya siasa vya mrengo wa kushoto vimewasilisha muswada wa kutokuwa na imani na serikali ya kihafidhina wiki hii vikiituhumu kujaribu kuficha ukweli baada ya treni ya mizigo kugongana na ya abiria katikati mwa Ugiriki mwaka jana, katika ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo ambapo watu 57 walifariki dunia.

Serikali inakanusha kutenda makosa yoyote na inatarajiwa kunusurika kutokana na wingi wa wabunge wa chama chake.

Lakini muswada huo unamulika namna watu wengi wanavyoendelea kukasirishwa na janga hilo lililodhihirisha namna miongo kadhaa ya kutelekezwa na usimamizi duni ilivyohatarisha usalama wa reli.

Wataalamu wanasema kumekuwepo na mabadiliko madogo sana kuboresha viwango tangu wakati huo.