Septemba 11.2001-miaka 6 iliopita | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Septemba 11.2001-miaka 6 iliopita

Leo ni Septemba 11 na ulimwengu unakumbuka siku hii miaka 6 iliopita pale jengo la World Trade Centre huko New York liliporipuliwa.

Bin Laden -je,nyuma ya septemba 11 ?

Bin Laden -je,nyuma ya septemba 11 ?

Leo ni Septemba 11-siku inayotukumbusha kutimu mwaka wa 6 tangu kutokea ile hujuma katika jingo la World Trade Centre,mjini New York na wizara ya ulinzi ya Marekani –PENTAGON mjini Washington.

Tangu siku hiyo,maisha yamaebadilika nchini Marekani na kwengineko ulimwenguni. Ukaguzi mkali katika viwanja vya ndege ndio athari kubwa zaidi ya tokeo lile.Isitoshe, haki za kiraia zimebanwa tangu pale rais George Bush kunadi vita dhidi ya ugaidi.

Rais George Bush hakukawia baada ya sham,bulio hilo la Septemba 11, 2001, miaka 6 iliopita kuimarisha mamlaka ya idara zake za usalama na ujasusi.Kwa mfano, wafungwa walibandikwa jina la “wapiganaji adui”-enemy combatants-ili kukwepa haki za kuwalinda chini ya mkataba wa Geneva.

Hata Bunge la Marekani-Congress lilikiukwa.

Haki za kiraia hazikutiwa tena maanani.Kupitia sheria kama vile “Patriot Act”,mawasiliano ya simu nay a mtandao wa Internat si mwiko tena kutosikiliza.

Isitoshe, haikuwa pia mwiko tena kujua akiba za mtu kwenye mabanki au wapi anatuma fedha.

Bibi Lisa Grawes ni makamo-mwenyekiti wa Taasisi ya taftioshi juu ya usalama wa taifa.Taasisi yake iliundwa 1974 ili kuchunguza idara za usalama zinaendesha kazi zao barabara na bila maonevu au kukanyaga haki za raia.

Anasema:

“Serikali hii ilijiamulia tena na mapema kutoomba ruhusa ya kutofanya hivyo.Haikuomba ruhusa si kabla ya kuwachunguza watu wala baadae .Tena imefanya hivyo, katika visa vingi.Idadi hasa haijulikani.Kwa namna hiyo, haki za mamia ya watu au hata maalfu nchini Marekani zilikanyagwa.”

Kwani, viongozi kama waziri wa sheria alietangaza atajiuzulu Septemba 17- zamani mshauri wa George Bush,Alberto Gonzalez,wakitoa hoja kuwa rais katika nyakati za dharura akihitaji madaraka ya aina hiyo.

Serikali ya rais Bush inajitetea sana kwamba sera zake zimesaidia kuzima hujuma zote kali dhidi ya marekani tangu Septemba 11, 2001.Mtaalamu wa sheria Mark Agrast anasema:

“Kwa mtu asieruhusiwa kujua habari za siri,ni vigumu kuikubali hoja hiyo.Lakini,kwa jicho la wamarekani wengi ,hatua zilizochukuliwa zinapindukia mahitaji ya usalama .”

Septemba 11,2001,utawala wa Bush uliamua kufuata mkondo huu ,anadai Agrast,kwani George Bush na makamo wake-rais Dick Cheney wameshika nyadhifa zao kwa nia kuimarisha madaraka ya rais-asema Agrast.

Hata wabunge wa Marekani wamekua wakikosoa mno .Tume ya Baraza la wakilishi ilidai wiki iliopita tu, wizara ya ulinzi nchini Marekani, iusimamioshe mradi wake ilioupanga uanze kazi mwezi ujao.Ni mpango wa kutumia vyombo vya satalaiti kuchunguza hata kinachopita ndani ya Marekani.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com