1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal yapitisha muswada wa msamaha

29 Februari 2024

Serikali ya Senegal imeukubali muswada wa msamaha unaolenga kuwaridhisha wapinzani, wakati ambapo nchi hiyo inakabiliana na mzozo wake mkubwa wa kisiasa kwa miongo kadhaa.

https://p.dw.com/p/4d0EP
Maandamano Senegal ya kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi
Polisi wakikabiliana na waandamanaji DakarPicha: John Wessels/AFP

Muswada huo wa msamaha ambao hadi upitia bunge, unaweza kupelekea kuachiwa kwa mamia ya watu waliozuiliwa na polisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yaliyozuka kwa mara ya kwanza mwaka 2021.

Kiongozi mkuu wa upinzani Ousmane Sonko, huenda akaachiwa huru pia. Muswada huo ulikuwa sehemu ya jawabu la Rais Macky Sall kwa mgogoro uliozuka baada ya hatua yake ya kuahirisha uchaguzi. Uchaguzi nchini Senegal ulikuwa unastahili kufanyika Jumapili iliyopita.