1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schuerrle arejea katika Ligi ya Premier

25 Julai 2018

Winga wa Ujerumani Andre Schuerrle anarudi katika Ligi ya Primier ya England kwa kujiunga na Fulham kwa mkopo kutoka klabu ya ligi kuu ya kandanda Ujerumani – Bundesliga

https://p.dw.com/p/324eh
Andre Schürrle
Picha: Getty Images/AFP/I. Kington

Wakala wa Schuerrle Ingo Haspel ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild kuwa mchezaji huyo amefanya vipimo vya matibabu katika klabu ya Fulham.

Jarida la Ujerumani – Kicker liliripoti kuwa uhamisho huo ni wa mkopo huku Dortmund ikimruhusu Schuerrle kurudi nyumbani kutoka ziara yao ya Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine.

Schuerrle aliwahi kuichezea klabu ya Chelsea kuanzia 2013-14. Fulham wamerudi katika ligi kuu ya Premier kwa kuapandishwa daraja msimu uliopita, baada ya kuwa katika daraja la pili kwa miaka minne.

Na mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Karim Bellarabi ameondoka hospitali siku moja baada ya kuzirai wakati wa mchuano wa kirafiki walioushinda ugenini dhidi ya Wuppertal.

Klabu hiyo ya Bundesliga imesema leo kuwa madaktari baada ya kufanya uchunguzi wa kina, wamesema sababu ya kuzirai kwake ilikuwa ni uchivu mwingi wa kimwili katika kipindi hiki cha joto kali. Mechi hiyo ya Jumanne ilichezwa katika wakati ambapo Ujerumani inashuhudia kiwango kikubwa cha joto kilichozidi nyuzijoto 30

Taarifa ya klabu hiyo imesema Bellarabi mwenye umri wa miaka 28 ataendelea kupata nafuu kwa siku kadhaa kabla ya kujiunga tena na wenzake mazoezini

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu