1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Scholz: Tutafanya juu chini kutatua mzozo wa bajeti

28 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameapa siku ya Jumanne kwamba serikali itafanya "kila linalowezekana" kutatua mzozo wa bajeti, lakini akueleza maelezo mengi namna atakavyofikia malengo.

https://p.dw.com/p/4ZX11
Berlin | Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa Bungeni
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa BungeniPicha: Lisi Niesner/REUTERS

Lakini Kansela Scholz hakueleza maelezo mengi juu ya jinsi atakavyofikia malengo yake ya kukuza nishati safi na kufanya uchumi wenye tija.

Wajerumani "wanahitaji uwazi katika nyakati zisizo na utulivu," Scholz alisema katika hotuba yake bungeni.

Aliahidi kuwa serikali haitaacha malengo ya kupunguza kwa kasi uzalishaji wa kaboni kutokana na nishati ya mafuta na kulinda matumizi ya kijamii.

Akizungumza katikati ya milipuko ya vicheko vya kejeli kutoka kwa wanachama wa upinzani, Scholz alisema litakuwa "kosa kubwa, lisilosameheka kupuuza uboreshaji wa nchi yetu."

Soma pia:Scholz alihutubia bunge la Ujerumani kuhusu mgogoro wa bajeti

Katika kupunguza matumizi kiwango maalum cha matumizi ya kawaida hakihitajiki tena kwa sababu bei ya nishati imepungua, ijapokuwa serikali inaweza kuchukua hatua zaidi ikiwa itapanda, Alisema Scholz mbele ya wabunge akinukuu wimbi wa kingereza unaokwenda kwa jina "You'll never walk alone."

Mjadala wa saa mbili bungeni umepangwa kufuatia hotuba ya Kansela huyo , kambi ya upinzani itaishambulia serikali kwa kujaribu kutafuta njia za kusimamisha utekelezaji wa ibara ya katiba inayoweka ukomo wa deni la taifa.

Sheria ya ukomo wa deni Ujerumani

Angela Merkel alipokuwa kansela mwaka wa 2009, Ujerumani iliweka kile kinachojulikana kama "ukomo wa deni" katika katiba yake.

Uchumi | Waziri wa Fedha Ujerumani  Christian Lindner
Waziri wa Fedha Ujerumani Christian Lindner Picha: Political-Moments/IMAGO

Hii inafidia nakisi ya bajeti ya serikali katika asilimia 0.35 ya pato la taifa, na ni ishara ya kujitolea kwa Ujerumani kufikia bajeti zilizosawazishwa inayojulikana kama "schwarze Null", kwa lugha ya kawaida unaweza kusema "sifuri nyeusi".

Wazo la vikwazo vikali vya matumizi lilipata nguvu mwanzoni mwa miaka ya 2000, na wanasiasa walichochewa kuchukua hatua za dhati kutokana na mzozo wa kifedha wa 2007-2008, wakati deni na nakisi ilipoongezeka.

Hatua hiyo inaweza kusimamishwa katika dharura, alimradi bunge litaunga mkono hoja hiyo.

Soma pia:Serikali ya Ujerumani yaidhinisha bajeti ya ziada na kuepusha mgogoro

Hii ilitokea katika mwaka wa 2020 hadi 2022, pale serikali ya Ujerumani ilipojitoa katika kukabiliana na janga la virusi vya Uviko-19, pia mzozo wa nishati uliyosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Ilitakiwa kuanza kutumika tena mwaka huu lakini kutokana na msukosuko wa bajeti, Waziri wa Fedha Christian Lindner alitangaza wiki iliyopita kuwa muungano huo ulikuwa unatafuta kughailisha kwa mara nyingine.

Mkwamo kutoka Mahakama ya Kikatiba

Mnamo Novemba 15, Mahakama ya Kikatiba ya Ujerumani iliamua kwamba serikali ya muungano inayoongozwa na Kansela Scholz ulichukua hatua kinyume na "ukomo wa deni", ikiwa ni hatua ya kujibu malalamiko ya kisheria yaliotolewa na vyama vya upinzani vya kihafidhina vya CDU na CSU.

Hukumu hiyo ilihusiana na uamuzi wa 2022 wa kuhamisha euro bilioni 60 ambazo zingeliweza kukopwa kwa malengo ya kukabiliana na athari za janga la UVIKO-19 pamoja na "mfuko wa mabadiliko ya hali ya hewa".

Athari ya moja kwa moja ya uamuzi huo ilikuwa kufuta kiasi cha euro bilioni 60 kutoka kwenye mfuko wa fedha za kukabiliana na hali ya hewa, ambayo ilikuwa na thamani ya euro bilioni 212.

Ukali wa maisha nchini Ujerumani

Soma pia:Rungu la Mahakama latikisa sehemu ya bajeti ya Ujerumani

Hatua hii inaweza kuathiri miradi ya maendeleo inayolenga kuharakisha hatua ya mpito ya Ujerumani kuelekea uchumi usio changia chafuzi wa hali ya hewa, kama vile uwekezaji mkubwa katika miradi ya umeme iliyotangazwa hivi karibuni.

Lakini uamuzi huo pia unaathiri fedha zingine "zisizo na bajeti", huku serikali sasa ikilazimika kuwajibika kwa matumizi ya ziada katika bajeti yake kuu.

Miradi iliokuwa chini ya mfuko wa hali ya hewa na mabadiliko ilisitishwa, ikifuatiwa na kughailishwa kwa matumizi yake kwa siku zijazo.

Waziri wa Fedha Lindner amelazimika kutaka tena kusimamisha ukomo wa deni, ikiwa ni pigo kubwa kwa FDP ambayo inaunga mkono hatua hizo.

Akitangaza taarifa ya maendeleo wiki iliyopita, hakusema lolote kuhusu "ukomo wa deni" badala yake alirejelea kwa mafumbo kuanzishwa kwa "bajeti ya nyongeza", na alishindwa kufafanua zaidi. Wakati huo huo mazungumzo kuhusu bajeti ya 2024 yapo katika mkwamo.

Yaliopewa kipaumbele katika bajeti 2024

Katika miaka ijayo, mkopeshaji mkubwa wa Ujerumani Benki ya LBBW inaamini kwamba matumizi makubwa ya ziada yatahitajika katika maeneo kadhaa ikiwemo ulinzi, pensheni na huduma za afya, vikiwa na uwezekano wa kufikia takriban asilimia tano ya Pato la Taifa.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa Bungeni
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa BungeniPicha: Hannibal Hanschke/REUTERS

Mchumi Mbobezi wa benki hiyo Moritz Kraemer alisema ili ujerumani kuweza kulinda nguvu yake ya kiuchumilazima kujiwekea "ukomo wa deni".

Lakini wakati chama cha Scholz SPD na chama cha Kijani vinania ya kulegeza sheria, chama cha FDP cha waziri Lindner kimeonekana kudhamiria kuweka ukomo wa deni. Wakati huo huo, ongezeko la  kodi ni mstari mwekundu kwa FDP.

Soma pia:Bunge la Ujerumani laidhinisha bajeti kubwa kwa jeshi

Katika dokezo la mzozo ndani ya muungano huo, Waziri wa Uchumi Robert Habeck kutoka chama cha Kijani alisema siku ya Jumatatu kwamba "miradi yote ilioanzishwa lazima iendelee."

Upinzani nao, umeelezea uamuzi huo kama "janga la kisiasa".

Siku ya Jumatatu Markus Soeder, kiongozi mwenye nguvu wa chama cha CSU, alipaza sauti kwa kutoa wito wa kufanyika  uchaguzi mpya wa shirikisho.