1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schick awanyemelea Lewandowski na Haaland

4 Oktoba 2021

Kwa sasa Patrick Schick anawanyemelea Erling Haaland na Robert Lewandowski kwenye kilele cha wafungaji bora wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa kuwa ana mabao sita huku Lewandowski na Haaland wakiwa na mabao saba kila mmoja.

https://p.dw.com/p/41FES
Bundesliga | Bayer Leverkusen - Borussia Dortmund
Picha: Tim Rehbein/RHR-FOTO/imago images

Haaland lakini ana jeraha na haibainiki iwapo atapatikana kwa mechi ijayo ya Dortmund naye Lewandowski amekwenda mechi mbili za ligi mfululizo sasa bila kufunga.

Tuzo ya mfungaji bora wa Bundesliga huitwa Törjägerkanone tafsiri yake ikiwa "tuzo ya muwindaji bora wa magoli."