Schalke yapata ushindi na kusonga hadi nafasi ya pili | Michezo | DW | 30.11.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Schalke yapata ushindi na kusonga hadi nafasi ya pili

Schalke imepanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya kandanda Ujerumani - Bundesliga pointi sawa na vinara Borussia Moenchengladbach baada ya ushindi wa 2 - 1 dhidi ya wageni Union Berlin

Schalke wana pointi 25 ijapokuwa na tofauti ndogo ya mabao ikilinganishwa na Gladbach, ambao watashuka dimbani Jumapili dhidi ya Freiburg. Katika mechi za leo, mabingwa Bayern Munich watakuwa nyumbani kuvaana na Bayer Leverkusen, wakati Jurgen Klinsmann ataanza enzi yake ya ukocha katika klabu ya Hertha Berlin nyumbani dhidi ya Borussia Dortmund. Mechi hii italetwa kwako moja kwa moja kupitia Idhaa ya Kiswahili ya DW.