Schalke wamfungisha virago Christian Gross | Michezo | DW | 01.03.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Schalke wamfungisha virago Christian Gross

Schalke 04 Jumapili walimuachisha kazi kocha wao Christian Gross baada ya msururu wa matokeo mabaya ikiwemo kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa VfB Stuttgart mwishoni mwa wiki.

Mechi nyengine iliyochangia ni ile ya dabi walipochapwa 4-0 na Borussia Dortmund wiki mbili zilizopita.

Ripoti zinaarifu kuna misukosuko ndani ya klabu hiyo na Gross pamoja na mwanachama wa bodi hiyo Jochen Schneider pamoja na Rainer Widmayer ambaye alikuwa kocha msaidizi wameachishwa kazi.

Haya yote yanakuja wakati ambapo kuna ripoti zinazosema baadhi ya wachezaji walikuwa wameitaka klabu hiyo kumuondoa uongozini Gross ambaye aliajiriwa Disemba mwaka jana.