1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schalke 04 yawaomba radhi mashabiki wake

Deo Kaji Makomba
4 Juni 2020

Klabu ya soka ya Schalke 04 inayoshiriki ligi ya Bundesliga, imeomba radhi mashabiki wake waliokuwa wamenunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia mechi ambazo hata hivyo hawakuweza kuhudhuria.

https://p.dw.com/p/3dGpm
FC Schalke 04 - SpVgg Unterhaching 5-3
Mashabiki wa klabu ya SchalkePicha: picture-alliance/Sven Simon

Wakati hekaheka za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani zikirejea tena baada ya kusimamishwa kufuatia mripuko wa virusi vya Corona, uongozi wa klabu ya soka ya Schalke 04 inayoshiriki ligi hiyo, Alhamis tarehe 04.06.2020 imeomba radhi kwa fomu ya kurejesha na isiyo na hisia baada ya kuwataka wapenzi na mashabiki wake waliokuwa wamenunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia mechi ambazo hata hivyo hawakuweza kuhudhuria kufuatia kutokea kwa janga la Covid 19, kuelezea ni kwa nini wanahitaji kurudishiwa pesa zao.

Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, ilisitishwa kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na janga hilo na kuanza tena katika viwanja vitupu kuanzia Mei 16 ili kupunguza hatari ya maambukizi mapya ya virusi vya corona.

Vilabu vya soka vimewapa marejesho mashabiki wao na kuponi kwa tiketi zao na wamiliki wengi wa tiketi za msimu Ujerumani wameamua kutouliza kurejeshewa pesa zao ili kusaidia vilabu vyao kifedha wakati wa kuwekwa kwa sheria ya karantini.

Lakini klabu ya Schalke 04 ilikwenda hatua ya mbele zaidi kuwataka mashabiki wake kuelezea sababu zao za kutaka kulipwa pesa kama vile hali ngumu ya kiuchumi na kuwasilisha nyaraka zinazounga mkono.

"Kwa nini unahitaji pesa sasa? Fafanua juu ya kesi yako na ugumu na ikiwezekana uwasilishe nyaraka husika," ilieleza barua ya klabu hiyo kwenda kwa mashabiki.

Hatua hiyo ilisababisha malalamiko ya haraka na kuufanya uongozi wa klabu ya Schalke 04 kuomba radhi. "Hakuna atakayehitaji kutoa hati na kwa kweli hakuna mtu atakayedhibitiwa," klabu hiyo ilisema katika taarifa yake.

"Katika barua kwa mashabiki wake, Schalke alitumia hisia zisizo za mtu na sio nyeti sana. Kwa hiyo klabu na wafanyakazi wa kituo cha huduma wangependa kuomba radhi kwa mashabiki wote. Tunaweza na tunapaswa kuonyesha vyema zaidi."

Mbali na matatizo ya kifedha, Schalke pia iko katika nafasi ya chini dimbani ikiwa haijashinda mechi zake 11 za mwisho huku ikikalia nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi hiyo ya Bundesliga.

Chanzo/RTRE