Sane afanya mazoezi ya kwanza na klabu ya Bayern Munich | Michezo | DW | 13.07.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Sane afanya mazoezi ya kwanza na klabu ya Bayern Munich

Mchezaji mpya Leroy Sane aliyesainiwa na klabu ya Bayern Munich, amefanya mazoezi yake ya kwanza Jumatatu na mabingwa hao wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga.

Winga Sane, ambaye alijiunga na Bayern akitokea Manchester City siku 10 zilizopita, aliambatana na Niklas Suele ambaye amerejea baada ya kupata majeraha ya goti.

Kikosi kizima cha Bayern kipo mapumzikoni kwa wiki mbili sasa baada ya kumaliza msimu wa mechi za ndani kabla ya kuanza maandalizi ya mechi za klabu bingwa Ulaya, ikianza na mechi ya pili ya hatua ya 16 bora dhidi ya Chelsea mnamo Agosti 8.

Bayern walishinda mechi ya kwanza kwa mabao 3-0. Hata hivyo Sane hatoweza kuichezea Munich katika michuano hiyo ya Champions League.