Sanaa:Wayemen warejeshwa nyumbani kutoka Guantanamo | Habari za Ulimwengu | DW | 18.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Sanaa:Wayemen warejeshwa nyumbani kutoka Guantanamo

Raia sita wa Yemen waliokua wakizuiliwa katika kambi ya kijeshi ya Marekani huko Guantanamo wamerudishwa nchini Yemen. Shirika la habari la nchi hiyo SABA halikutoa maelezo zaidi juu ya kuachiwa kwa wafungwa hao, au kama watafunguliwa mashitaka nchini Yemen. Shirika hilo lilinukulu tu duru kutoka wizara ya ndani ikisema kuna mawasiliano na maafisa wa Marekani juu ya kuachiwa kwa Wayemen hao kutoka Guantanamo. Jana wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema jumla ya wafungwa 18 katika jela ya Guantanamo wamerejeshwa katika nchi zao mwishoni mwa juma na kupunguza idadi ya wanaendelea kushikiliwa kuwa 395. Kwa mujibu wa tarakimu zisizo rasmi, idadi ya raia wa Yemen wanaozuiliwa katika gereza la Guantanamo ni 130.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com