1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Samatta awaomba mashabiki kutoishambulia timu yake

3 Februari 2020

Mshambuliaji wa Aston Villa Mtanzania Mbwana Samatta amewaomba mashabiki wake kutoandika ujumbe au maoni yao kwa kutumia lugha chafu kwenye akaunti za mitandao ya kijamii ya wachezaji au vilabu.

https://p.dw.com/p/3XDIb
UK Premierleague Samatta
Picha: AFP/P. Ellis

Samagoal kama anavyofahamika ameandika kwenye mitandao yake ya kijamii kuwa na namnukuu "Mashabiki wa soka Tanzania nafaham kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vzr ktk timu yangu mpya,lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika ac/ za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi".

Samatta, 27, ametoa kauli hiyo kufuatia maneno ya kashfa yanayotolewa kwa lugha ya kiswahili kwenye akaunti za timu ya Aston Villa pamoja na baadhi ya wachezaji kama Grealish. Samatta alifunga bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza ya Premier League tangu alipojiunga na Aston Villa akitokea Genk ya Ubelgiji.