Salazar akanusha tuhuma za dawa za kulevya | Michezo | DW | 09.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Salazar akanusha tuhuma za dawa za kulevya

Kocha wa riadha Mmarekani Alberto Salazar amekana shutuma dhidi yake kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni akisema kuwa wanaomtuhumu “wanafahamu wazi kuwa wanatoa kauli za uongo

Salazar anayemfundisha mwanariadha wa Uingereza Mo Farah nchini Marekani, amekana tuhuma zilizotolewa na uchunguzi wa BBC katika uchunguzi wake, kuwa alitumia mbinu zisizokubalika.

Hakuna shutuma zozote zinazomhusisha Farah na matumizi ya dawa hizo isipokuwa mwenyekiti wa chama cha riadha cha Uingereza Ed Warner amesema kuwa data za damu za mwanariadha huyo zitafanyiwa uchunguzi.

Uchunguzi wa BBC ulidai kuwa Salazar ambaye alikuwa Kocha wa Farah mwaka 2011, alikiuka sheria zinazopinga dawa zilizopigwa marufuku michezoni na alimpatia dawa hizo, bingwa wa mbio za mita 10,000 Galen Rupp wa Marekani alipokuwa na umri wa miaka 16 mwaka 2002.

Mwandishi: Bruce Amani/Rueters
Mhariri: Yusuf Saumu