Rwanda: Mamlaka ya Magereza yaitaka serikali iwaachie wafungwa wazee | Matukio ya Afrika | DW | 04.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Rwanda: Mamlaka ya Magereza yaitaka serikali iwaachie wafungwa wazee

Mamlaka ya magereza nchini Rwanda yameitaka serikali ya nchi hiyo kuwaachia wafungwa zaidi ya 2000 ambao wanakabiliwa na tatizo la uzee linalowasababishia kupoteza maisha yao kutokana na maradhi.

Wazee Wakongwe wanapoteza maisha kwenye magereza ya Rwanda

Wazee Wakongwe wanapoteza maisha kwenye magereza ya Rwanda

Mamlaka hiyo imesema zaidi ya asilimia 60 ya mahabusu wanaopoteza maisha kwenye magereza ya Rwanda ni wazee wakongwe wenye umri zaidi ya 70. Mamlaka ya magereza yanasema kwamba mwito unawahusu hata mahabusu wa mauaji ya kimbari ya mwaka 94 nchini Rwanda.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi.

(Kusikiliza ripoti bonyeza alama ya spika za masikioni)

Mwandishi: Sylvanus Kalemera

Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada