1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiRwanda

Rwanda : Denis Kazungu ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Tatu Karema
9 Machi 2024

Raia wa Rwanda Denis Kazungu amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuwaua watu 14 katika mfululizo wa mauaji ya kupanga

https://p.dw.com/p/4dKnK
Mahakama ya juu ya Kenya
Mahakama ya juu ya KenyaPicha: John Ochieng/SOPA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Kazungu mwenye umri wa miaka 34 ambaye awali aliomba msamaha na hukumu ndogo, hakuwepo mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo na haijafahamika mara moja ikiwa atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Soma pia:Mahakama ya Rwanda yaamuru Kazungu kuzuiliwa kwa siku nyengine 30

Kazungu alikuwa amekiri makosa 10 ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji, kughushi na kuharibu maiti.

Duru ya polisi imearifu shirika la habari la AFP kwamba Kazungu alikiri kwamba alijifunza kuwauwa waathiriwa wake wengi wao makahaba kwa kutazama filamu za wauaji sugu.