Russia katika Olimpik | Michezo | DW | 25.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Russia katika Olimpik

Russia imepania kuzipiku kwa medali Marekani na wenyeji China katika michezo ya Beijing.

ssia, zamani Urusi, ni mojawapo ya dola kuu za kispoti na katika michezo ya olimpik,Russia imekuwa likishindana na Marekani ili kuparamia kileleni mwa orodha ya medali za dhahabu,fedha na shaba katika medani ya olimpik .

Katika michezo ijayo ya olimpik ya Beijing inayoanza August 8 hadi 24, Russia itapewa changamoto kali sio tu na hasimu yake mkubwa Marekani, bali hata wenyeji China.

China imekamia kuzuwia jogoo la shamba-Marekani na Russia, kuwika mjini Beijing.

►◄

Wanariadha wa Russia-wake kwa waume wamepania kurejea Moscow kutoka Beijing na medali zaidi za olimpik kuliko ilivyofanya miaka 4 iliopita huko Athens,Ugiriki ilipokuja nyuma ya Marekani na China.

Mwenyekiti wa Kamati ya olimpik ya Russia Leonied Tyagachev alinukuliwa kusema majuzi,

"Itakua kazi ngumu kuzipiku katika orodha ya medali nchi kama Marekani na china. Lakini, wanariadha wetu wamejiandaa uzuri na naamini tutafanya uzuri Beijing na kujipatia matokeo bora zaidi kuliko miaka 4 iliopita."-alisema Leonied Tyagachev.

Huko Athens, Russia imetokea 3 baada ya kuhodhi medali 92 kati ya hizo 27 za dhahabu,27 za fedha na 38 za shaba.

Mkuu huyo wa Kamati ya olimpik ya russia anatazamia russia kutamba zaidi katika mashindano yanayotumia mpira ambamo timu za Russia na wanariadha wake wametia fora karibuni.

Timu za Russia tangu ile ya wanaume hata ya wanawake iltwaa ubingwa wa mchezo wa basketball wa Ulaya na zinapigiwa debe kutwaa medali za dhahabu katika Olimpik.

Katika Volleyball pia timu zote mbili za akina kaka na akina dada za russia zinatumainiwa kushinda.

timu ya wasichana wa Russia ya mpira wa mkono-handball ni mabingwa wa dunia halkadhalika, inatarajiwa kutamba wakati .

katika medani ya tennis upande wa wanawake, Russia ina matumaini makuu ya kunyakua medali kwavile wasichana wa Russia wamekuwa kileleni mwa mashindano ya WTA.

Nyota ya russia wa Tennis Maria Sharapova,Svetlana Kuznetsova,Elena Dementieva na dinara safina wote wana uwezo wa kutwaa medali za dhahabu huko Beijing.

Russia inatazamia pia medali kutoka medani ya riadha:katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi wanawake, Russia inamtarajia Yekaterina Volkova kuwika a na km 20 Olga Kaniskina ni maarufu.

Katika kuruka juu kw upongoo (Pole vault) hakuna shaka yoyote,Yelena Isinbayeva ni malkia na atarudi tena kama miaka 4 nyuma huko Athens na medali ya dhahabu hadi Moscow.

Tatiana Lebedeva ni malkia katika longo jump. Hii inafuatia ushindi wake wa medali ya dhahabu katika mashindano ya mwaka jana ya ubingwa wa riadha ulimwenguni huko Osaka,Japan.

Katika kikosi chake cha wanaume, Russia inaweka matumaini ya ushindi wa medali kwa bingwa wa olimpik wa mita 800 huko Athens, Yury Borzakovsky.

Kuna matumaini yasio wazi ya ushindi kwa Rybakov katika high jump,Sergei Makarov katika kurusha mkuki (javelin) na katika kuruka kwa upongooYevgeny Lukianenko ameruka mita 6.1 mapema mwezi huu.

Russia inatumai pia kutamba katika mashindano ya miereka ya olimpik-wrestling.Halkadhalika, mabondia wake wanaotamba katika ringi ya ulaya ya wapiganaji wasiolipwa,wanatazamniwa kuongeza uzito katika nguvu zake sawa na waogoleaji wake,gymnasts na watunga-shabaha.

Russia imejiwinda kweli kuzipiku Marekani na China.Ikiwa shabaha yake hii itaweza kuifikia, yafaa kusubiri na kuona.