Rummenige: Bundesliga lazima ikaze buti | Michezo | DW | 17.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Rummenige: Bundesliga lazima ikaze buti

Kiongozi wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenige ameonya kuwa kandanda la Ujerumani na vilabu vya Bundesliga vinapaswa kuwa makini au vitabakia nyuma katika soko la kimataifa

Rummenige amesema shughuli za soko la uhamisho wa wachezaji zinaonyesha wazi namna mambo yanavyokwenda nchini England. Amesema Bundelsiga lazima iwe chonjo ili isinunuliwe na England.

Premier League ya England hutumia fedha nyingi zaidi kuliko ligi nyingine yoyote Ulaya. Kandarasi mpya ya matangazo ya televisheni kwa ajili ya misimu ya mwaka wa 2016 hadi 2019 itatoa euro bilioni 6.9 kwa vilabu 20 vya ligi hiyo. Bundesliga kwa sasa inatengeneza euro bilioni 2.5 kutoka kwa mkataba wake wa matangazo ya televisheni wa miaka minne.

Rummenigge anasema Bundesliga lazima ipiganie nafasi ya kujionesha zaidi katika mataifa ya ng'ambo, na ndio maana Bayern Munich iko ziarani China wakati Borussia Dortmund ikitua nchini Singapore wakati wa maandalizi yake ya kucheza Malaysia na Japan.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdul-Rahman