1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uhuru wa vyombo vya habari

RSF: Jitihada zaidi zinahitajika kuimarisha uhuru wa habari

3 Mei 2024

Shirika la kutetea haki za waandishi wa habari la "Reporters Without Borders" limeonya juu ya serikali kupunguza juhudi za kuunga mkono uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4fT86
Uhuru wa Vyombo bya habari
Mei 3 Ulimwengu unaadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo bya habariPicha: Nyein Chan Naing/dpa/picture alliance

Shirika hilo limesema hayo katika ripoti ya mwaka ya takwimu za uhuru wa vyombo vya habari.  

Takwimu hizo zinaonesha Norway kuendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa kuwa na uhuru wa habari, huku Eritrea ikiwa nafasi ya mwisho iliyoshikiliwa na Korea Kaskazini mwaka uliopita. 

RSF yamshutumu rais wa Mexico kwa kushindwa kuwalipa waandishi wa habari

Miongoni mwa nchi kumi zilizopo nafasi za mwisho kulingana na ripoti hiyo ni China, Iran, Korea Kaskazini, Syria na Eritrea. 

Shirika hilo pia limeonya kwamba wanasiasa katika mataifa mengi wamekuwa wakiminya uhuru wa habari na kuchochea chuki dhidi ya waandishi wa habari kwa kuwafanya watu wasiwaamini na kwa kuwatisha.