1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robben arejea dimbani katika timu yake ya zamani

Admin.WagnerD29 Juni 2020

Hebu sikiliza hii. Kama wewe ni mpenzi wa kandanda basi jina la Arjen Robben sio jipya kwako. Sasa, winga huyo wa kimataifa wa Uholanzi amejiunga na la klabu yake ya kwanza kabisa FC Groningen.

https://p.dw.com/p/3eWOX
Fußball 1. Bundesliga 2019 | FC Bayern München | Arjen Robben
Picha: picture-alliance/augenklick/firo Sportphoto/S. El-Saqqa

Na mojawapo ya sababu za kujiunga nayo ni "mapenzi ya klabu”. Robben mwenye umri wa miaka 36 aliondoka Bayern Munich mwaka mmoja uliopita na kutangaza kutundika daluga. "Kwa sasa, nadhani imepokelewa vizuri na watu hapa na ndio maana lazima iwe wazi na nitabaki kuwa wazi kuhusu hilo katika wiki zijazo na miezi, au huenda safari hii ikaisha baada ya mwezi mmoja lakini labda itaisha miaka miwili kutoka sasa. Au katikati ya hapo. huenda." Amesema Robben

Winga huyo pia aliwahi kuzichezea Chelsea, PSV Eindhoven na Real Madrid, huku akishinda mataji 12 ya ligi na kucheza mechi 96 za timu za taifa ikiwa ni pamoja na fainali ya Kombe la Dunia la 2010 mjini Johanesburg.