Ribery arejea mazoezini baada ya miezi tisa
4 Desemba 2015Matangazo
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anatumai kucheza katika kikosi cha kwanza mnamo Desemba 12 katika mchuano kati ya Bayern na Ingolstadt.
Kocha wa Bayern Pep Guardiola amefurahishwa na habari za kurejea Ribery, akisema hatamharakisha kurejea kikosini hadi atakapokuwa katika hali nzuri kabisa kucheza
Ribery alikuwa mkekani kwa siku 264 kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu ambayo yamemtatiza mara kwa mara tangu alipoyapata mnamo Machi 11 mwaka huu. Chipukizi wa Kifaransa Kingsley Coman amekuwa akifanya vyema sana kulijaza pengo la Ribery
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/reuters
Mhariri: Josephat Charo