1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RB Leipzig yatinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa

Bruce Amani
14 Agosti 2020

Klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani - Bundesliga RB Leipzig imetinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Atletico Madrid 2 - 1 katika mashindano yanayoendelea mjini Lisbon, Ureno

https://p.dw.com/p/3gwWf
Portugal | Champions League - Viertelfinale - RB Leipzig - Atletico Madrid
Picha: Reuters/L. Gene

Klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ujerumani - Bundesliga RB Leipzig imetinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Atletico Madrid 2 - 1 katika mashindano yanayoendelea mjini Lisbon, Ureno.

Timu hiyo ya Kocha Julian Nagelsmann ilipata ushindi huo baada ya kuonyesha mchezo mzuri dhidi ya miamba hao wa Uhispania, licha ya kutokuwa na mshambuliaji wao nyota Timo Werner aliyehamia klabu ya Chelsea nchini England. Leipzig sasa itakutana na Paris Saint-Germain Jumanne ijayo.

PSG inayofundishwa na Mjerumani Thomas Tuchel iliipiga Atalanta Bergamo 2 - 1 katika dakika ya mwisho siku ya Jumatano. Hii leo, mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich watashuka dimbani dhidi ya miamba ya Uhispania FC Barcelona.