Ratiba ya msimu wa 2015/2016 wa ligi ya England yatolewa | Michezo | DW | 17.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ratiba ya msimu wa 2015/2016 wa ligi ya England yatolewa

Ratiba ya michuano ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England – Premier Legaue, imetolewa ambapo Chelsea itaanza kulitetea taji lao nyumbani dhidi ya Swansea wikendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti

Manchester City iliomaliza katika nafasi ya pili pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.

Arsenal itaialika West Ham, Liverpool itaenda Stoke katika mchuano unatarajiwa kuwa mgumu, Newcastle itakabiliana na Southampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.

Bournemouth iliopandishwa daraja msimu huu, Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa, Everton na Crystal Palace mtawalia.

Msimu huu wa 2015/2016 utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohamed Khelef