1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTogo

Rais wa Togo aidhinisha sheria ya kurefusha uongozi wake

7 Mei 2024

Rais wa Togo Faure Gnassingbe ameidhinisha katiba mpya yenye utata ambayo sasa wananchi sio watakaopiga kura kumchagua rais nchini humo.

https://p.dw.com/p/4fayv
Faure Gnassingbé
Gnassingbe ambaye ameiongoza Togo kwa miaka 19, alimrithi baba yake Gnassingbe EyademaPicha: Filip Singer/EPA POOL/dpa/picture alliance

Wakosoaji wanasema sheria hiyo mpya itamuwezesha Gnassingbe kusalia madarakani na kuuendeleza utawala wa familia yake ambayo imekuwa madarakani kwa muda wa miaka 60 hadi sasa.

Soma pia: Waangalizi wasema uchaguzi wa Togo ulikuwa huru

Hayo yanajiri wakati Tume ya uchaguzi nchini Togo imetangaza kuwa chama tawala cha Rais Gnassingbe Cha UNIR kimeshinda uchaguzi wa Bunge kwa kujikusanyia jumla ya viti 108 kati ya 113.

Gnassingbe ambaye ameiongoza Togo kwa miaka 19, alimrithi baba yake Gnassingbe Eyadema, ambaye alitawala kwa takriban miongo minne nchi hiyo ndogo ya pwani ya Afrika Magharibi inayopatikana kati ya mataifa ya Benin na Ghana.