1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais wa Taiwan azuru Amerika ya Kati kutafuta ushirika zaidi

1 Aprili 2023

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen amewasili nchini Guatemala kwa ziara inayokusudia kuimarisha uhusiano na washirika wake wanaopungua kufuatia ziara ya Marekani iliyoikasirisha China.

https://p.dw.com/p/4PaIi
Guatemala | Ankunft von der taiwanesische Präsidentin Tsai Ing-wen
Picha: Guatemala's Presidency/Handout/AFP

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen amewasili nchini Guatemala kwa ziara inayokusudia kuimarisha uhusiano na washirika wake wanaopungua kufuatia ziara ya Marekani iliyoikasirisha China. Ziara ya Tsai nchini Guatemala na jirani yake Belize katika kanda ya Amerika ya Kati inafanyika baada ya Honduras kujiunga na mataifa yaliyokata uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan na kuegemea upande wa China. Akiwa njiani, Rais Tsai alipitia mjini New York, Marekani, na kutangaza mipango ya kukutana na Spika wa Bunge la Marekani, Kevin McCarthy. Marekani ilisema hapakuwa na sababu kwa China kuchukia safari ya kawaida, lakini Beijing imeionya Washington kwamba inacheza na moto. Tsai aliwasili Guatemala siku ya Ijumaa mchana na kufanya mkutano mfupi na Rais wa nchi hiyo, Alejandro Giammattei, ambaye serikali yake imeitangaza Taiwan kuwa ndiyo "China pekee na ya kweli."