1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Senegal aapa kuheshimu uamuzi wa baraza la katiba

Sylvia Mwehozi
17 Februari 2024

Rais wa Senegal Macky Sall, ambaye anakabiliwa na shinikizo kubwa la ndani na nje ya nchi, ameapa kuandaa uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo baada ya baraza kuu la kikatiba kubatilisha uamuzi wa kuchelewesha uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4cVkK
Senegal I Macky Sall
Rais wa Senegal Macky SallPicha: Amr Alfiky/File Photo/REUTERS

Rais wa Senegal Macky Sall, ambaye anakabiliwa na shinikizo kubwa la ndani na nje ya nchi, ameapa kuandaa uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo baada yabaraza kuu la kikatiba kubatilisha uamuzi wake wa kuchelewesha uchaguziwa mwezi huu.

Ofisi ya rais imesema kwamba Rais Sall anakusudia kutekeleza kikamilifu uamuzi wa baraza kuu la kikatiba na kwamba atafanya mashauriano muhimu ya kuandaa uchaguzi wa rais haraka inavyowezekana.

Uamuzi wa dakika ya mwisho wa Rais Sall wa kuchelewesha uchaguzi wa Februari 25, umeitumbukiza Senegal katika mzozo mbaya wa kisiasa. Baraza la kikatiba la nchi hiyo lilitoa uamuzi uliobatilisha kura ya bunge ya kuunga mkono tangazo la kuchelewesha uchaguzi, likisema ilikuwa kinyume na katiba.