Rais Poroshenko, kuzungumza kwa simu na Vladimir Putin | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.06.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Rais Poroshenko, kuzungumza kwa simu na Vladimir Putin

Rais mpya wa Ukraine amepata uungwaji mkono na viongozi wa Ujerumani na Ufaransa kuhusiana na mpango wa mazungumzo ya simu leo(29.06.2014) na rais wa Urusi Putin wakati muda wa mwisho wa kusitisha mapigano unakaribia.

Ukraine Präsident Petro Poroschenko Vereidigung 07.06.2014 Player-Version

Rais Petro Poroshenko wa Ukraine

Na wakati huo huo wanamgambo wanaounga mkono Urusi wamewaacha huru waangalizi zaidi wa Ulaya.

Rais Petro Poroshenko anatarajia kujiunga na kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande katika mazungumzo hayo ya simu yaliyopangwa kuzungumza na rais wa Urusi katika mkesha wa kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano.

Ukrainischer Präsident Poroschenko und Kanzlerin Angela Merkel beim EU-Gipfel in Brüssel

Poroshenko akizungumza na kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Mazungumzo hayo ya simu leo (29.06.2014) kimsingi yanalenga kuangalia hatua zozote za mabadiliko kutoka Urusi kabla ya Umoja wa Ulaya na Marekani kufikiria kuweka vikwazo zaidi vitakavyokuwa vikali zaidi dhidi ya sekta za fedha na kijeshi nchini Urusi siku inayofuata.

Urusi itaunga mkono kusitisha mapigano?

Ukraine na washirika wake wa mataifa ya magharibi wamekuwa wakitafuta kuona hatua kamili kutoka Urusi kuunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo uongozi mjini Kiev umerefusha na wapiganaji siku ya Ijumaa kwa matumaini ya kutuliza mapigano yaliyosababisha maafa ambayo yamezuka kutokana na nchi hiyo kufuata njia mpya ya kuelekea katika mataifa ya magharibi.

Moskau Russland Präsident Wladimir Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin

Mazungumzo hayo ya simu pia yanakuja baada ya waasi wanaoiunga mkono Urusi katika eneo la mashariki ya Ukraine siku ya Jumamosi wamewaachia huru waangalizi wanne kutoka shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE) -- mwanamke mmoja na wanaume watatu-- baada ya kuwekewa mbinyo na rais Putin kutimiza masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Ukraine.

Waangalizi wa shirika hilo la OSCE walionekana wamechoka lakini wakiwa wanajisikia furaha wakati wakikabidhiwa kwa maafisa na kundi la wapiganaji ambao walikuwa na silaha nzito kwa mwakilishi wa kundi hilo katika hoteli katika eneo la mashariki la mji wa Donetsk.

"Tunawaacha huru waangalizi wa mwisho wanne ambao wamekuwa wakishikiliwa katika eneo la jamhuri ya watu wa Lugansk ," waziri mkuu wa jamhuri hiyo iliyojitangaza ya watu wa Donetsk amewaambia waandishi habari. "Tunaliona hilo kuwa ni kutimiza majukumu yetu yote," Oleksandr Borodai amesema.

Ukraine OSZE Beobachter freigelassen in Donezk

Waangalizi wa OSCE wakiwa huru

Kundi la kwanza la waangalizi waliokamatwa Mei 26 katika jimbo la Donetsk lilikabidhiwa kwa OSCE siku ya Alhamis.

Hatua ya kuachiliwa mateka yakaribishwa

Shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Vienna limesema kundi la pili linajumuisha watu kutoka Ujerumani, Uholanzi, Uhispania na Urusi. "Tunakaribisha hatua ya kurejea kwa waangalizi wa mwisho wanne ambao walikuwa wametekwa nyara wa kundi maalum la waangalizi wa OSCE baada ya mwezi mzima," naibu mkuu wa ujumbe huo nchini Ukraine, Mark Ethirington, amesema katika taarifa.

Kukamatwa kwa waangalizi wa OSCE kumeathiri kwa kiasi kikubwa operesheni za ujumbe huo katika eneo la mashariki ya Ukraine katika wakati upatikanaji wa taarifa muhimu ulikuwa muhimu zaidi."

Ukraine Konflikt OSZE Inspektoren

Waangalizi wa OSCE wakikagua mzozo wa Ukraine

Shirika la OSCE, lililoundwa na mataifa 57 katika miaka ya 1970 kuangalia usalama katika bara la Ulaya wakati wa enzi za vita baridi-- imechukua jukumu la juu katika kujaribu kupatanisha kwa mapigano ya wiki 12 katika jimbo hilo la zamani la iliyokuwa Umoja wa Kisoviet.

Ujerumani pia imezungumzia kuhusu kuachiliwa kwa kundi hilo la waangalizi wa OSCE, ikieleza furaha yake na kusisitiza haja ya kuendelea na usitishaji wa mapigano.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com