Rais Kibaki azuia mswada wa wabunge kujipatia marupurupu | Matukio ya Afrika | DW | 10.10.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Rais Kibaki azuia mswada wa wabunge kujipatia marupurupu

Rais wa Kenya, Mwai Kibaki ameuzuia mswada wa sheria ambao ungewawezesha wabunge kujipatia marupurupu kiasi cha dola 110,000 watakapomaliza mihula yao ya kazi bungeni mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya

Rais Mwai Kibaki wa Kenya

Uamuzi wa jana wa Kibaki ulifuatia kilio cha wananchi wakati nchi hiyo ikiwa imepandisha kodi zake kuziba pengo katika mahitaji yake ya fedha huku ikikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi. Josephat Charo amekusanya maoni ya baadhi ya wakenya kuhusu uamuzi wa rais Kibaki.

(Kusikiliza maoni hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada