1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qatar inatathmini jukumu lake la upatanishi Israel na Hamas

Hawa Bihoga
18 Aprili 2024

Qatar imesema inathmini tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas kutokana na kile ilichokesema, kuna mipaka katika jukumu hilo lililonuia kuleta amani katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4eu0Z
Qatar Doha | Antony Blinken na Mohammed Bin Abdulrahman katika picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Qatar Mohammed Bin Abdulrahman.Picha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje Mohammed bin Abdulrahman bila kutaja yeyote,amewaambia waandishi wa habari kwamba jukumu la Qatar limetumiwa vibaya na baadhi ya watu kutokana na ukomo wa maslahi ya kisiasa.

Aidha ameongeza kwamba hatua hiyo imeisababisha Qatar kufanya tathmini kamili juu ya jukumu lake lililofungamana na mukhtadha wa kibinaadamu. Hapo awali bin Abdulrahman alisema mazungumzo kati ya Israel na Hamas ya kutafuta makubaliano ya usitishwaji mapigano katika Ukanda wa Gaza yamekwama.

Soma pia:Kiongozi wa Hamas asema hakuna mabadiliko katika mazungumzo ya Cairo

Qatar, Marekani na Misri wamekuwa wakisimamia mazungumzo ya wiki kadhaa ambayo pia yangeliwezesha kuachiliwa kwa mateka wa Israel pamoja na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel.