1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin na Erdogan kujadili mzozo wa Syria

3 Desemba 2012

Makombora na ndege za kivita za Syria zimeshambulia maeneo ya waasi ndani na nje ya mji mkuu Damascus katika operesheni ya kuudhibiti mji huo,wakati Urusi na Uturuki zinajitayarisha kwa mazungumzo juu ya Syria.

https://p.dw.com/p/16uur
Russian Prime Minister Vladimir Putin (L) and Turkish Prime Minister Recep Tayyip Erdogan (R) shake hands during a joint news conference following their talks in Ankara, Turkey 06 August 2009. Russian Prime Minister Vladimir Putin and Turkish counterpart Recep Tayyip Erdogan signed on 06 August agreements on cooperation in the gas sphere, in particular, an agreement on the South Stream pipeline construction through the Turkish territorial waters. EPA/RIA NOVOSTI ALEXEY NIKOLSKY +++(c) dpa - Report+++
Rais wa Urusi Vladimir Putin na waziri mkuu wa Uturuki ErdoganPicha: picture-alliance/dpa

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton , wakati huo huo ametoa onyo kali kwa utawala wa rais Bashar al-Assad kuhusiana na uwezekano wa kutumia silaha za kimekali dhidi ya waasi.

Shirika linaloangalia haki za binadamu nchini Syria limesema kuwa makombora ya Syria yameshambulia maeneo katika wilaya ya Hajar al-Aswad na Tadamun pamoja na kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Yarmuk kusini mwa mji mkuu Damascus.

Putin akutana na Erdogan

Rais wa Urusi Vladimir Putin , wakati huo huo , alitarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wakati wa ziara ya kihistoria mjini Istanbul kujadili tofauti zao kuhusu Syria.

Mazungumzo hayo yametuwama katika "hali ya mapatano katika mashariki ya kati, hali katika ukanda wa Gaza, mzozo nchini Syria , pamoja na ushirikiano," mshauri ya masuala ya mambo ya kigeni wa Putin , Yury Ushakov amesema.

Uturuki na Urusi zimeingia katika mgongano kuhusiana na vipi inawezekana kuutatua mzozo nchini Syria ambapo serikali ya nchi hiyo inaendesha ukandamizaji wa wapinzani kwa nguvu na kusababisha umwagikaji mkubwa wa damu, licha ya ukuaji wa biashara pamoja na mahusiano katika sekta ya nishati.

Mvutano huo ulifikia kilele mwezi Oktoba mwaka huu baada ya Uturuki kuikamata ndege ya Syria iliyokuwa ikitokea Moscow kwenda Damascus , kwa tuhuma za kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba shehena ya silaha, na kusababisha jibu la hasira kutoka Urusi.

Watu 12 wauwawa

Mashambulio ya anga katika mji wa mpakani wa Ras al-Ain yamesababisha watu 12 kuuwawa na wengine zaidi ya 30 leo. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na watoto wanne na waasi wanane, limesema shirika la kuangalia haki za binadamu nchini Syria.

epa03488718 A handout picture released by the Syrian Arab News Agency (SANA), shows Syrian citizens inspecting the scene of a car bomb attack in Jaramana of Druze majority in Rural Damascus, Syria, 28 November 2012. According to SANA terrorists set off two explosions with two car bombs parked at the main square in the Jaramana neighborhood of rural Damascus. The blast led to a number of death and wounded citizens, and a large amount of damage to surrounding buildings, SANA also stated. EPA/SANA / HANDOUT HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mashambulio ya jeshi la Urusi mjini Damascus katika maeneo ya waasiPicha: picture-alliance/dpa

Hali hiyo imesababisha ndege za kivita za Uturuki kupelekwa haraka katika eneo la mpakani.

Duru za usalama zimesema kuwa ndege za kivita chapa F-16 za uturuki zilipelekwa haraka kutoka katika kituo chake katika mji wa kusini mashariki ya Diyarbakir baada ya mashambulio ya anga katika makao makuu ya jeshi la ukombozi wa Syria katika mji wa Ras al-Ain, ikiwa ni onyo kwa Syria kutokiuka sheria ya mkapa na kuingia nchini Uturuki.

epa03371099 A grab from a handout video made available by Shaam News network (SNN) on 27 August 2012, state to show a helicoper falling down following clashes between the Syrian Army and the Free Syrian army, near Damascus, Syria. According the state media, a Helicoper crashed in al-Qaboun district, close to Jobar. The free Syrian Army claimed they shot the aircraft. EPA/SNN HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FROM AN ALTERNATIVE SOURCE AND CANNOT PROVIDE CONFIRMATION OF CONTENT, AUTHENTICITY, PLACE, DATE AND SOURCE. HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mapambano hewani. Helikopta ya jeshi la Syria baada ya kushambuliwa na waasiPicha: picture-alliance/dpa

Waasi waliukamata mji huo kiasi mwezi mmoja uliopita katika mapigano ambayo yalisababisha makundi makubwa ya wakimbizi kuingia nchini Uturuki, na imekuwa ni jaribio katika uvumilivu wa Uturuki kuweza kujilinda dhidi ya ghasia kusambaa hadi katika ardhi yake.

Mwandishi: Sekione Kitojo/ rtre/afpe

Mhariri: Yusuf Saumu