PSG mabingwa mara 8 Ufaransa | Michezo | DW | 22.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

PSG mabingwa mara 8 Ufaransa

Paris Saint Germain walitawazwa ubingwa mara nane wa Ligue 1 ya Ufaransa kufuatia ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Monaco uwanjani Parc des Princes siku ya Jumapili.

Kylian Mbappe ndiye aliyefunga magoli yote matatu ila ilikuwa ni habari njema zaidi kwa PSG kwa kuwa nyota wao Neymar alirudi uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na jeraha la mguu.

Mbrazili huyo alicheza kipindi chote cha pili kwenye mtanange huo.

PSG wanaweza kushinda mataji mawili msimu huu iwapo watawalaza Stade Rennais katika fainali ya French Cup Jumamosi.