1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PSG dhidi ya Arsenal: Muda ndio utaamua

30 Mei 2026

PSG na Arsenal wanakutana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Budapest. PSG wanategemea mashambulizi yao makali huku Arsenal wakisaka taji lao la kwanza katika pambano linalosubiriwa kwa hamu.

https://p.dw.com/p/5Ea1X
Champions League –
Arsenal wanatafuta taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku PSG wakisaka kuwa klabu ya kwanza ya Ufaransa kutwaa kombe hilo mara mbili.Picha: Peter Cziborra/Action Images/REUTERS

Kadri saa zinavyosogea kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa mjini Budapest,  Paris Saint‑Germain wanajiandaa kuleta burudani kupitia safu yao ya ushambuliaji wakipambana dhidi ya safu imara ya ulinzi ya Arsenal, katika pambano linaloonekana kuwa la mitindo miwili tofauti.

Kocha wa PSG, Luis Enrique, amesema hakuna timu iliyo bora kuliko nyengine, akisisitiza kuwa matokeo yataamuliwa na maamuzi madogo ndani ya mchezo.

PSG wanaingia fainali hii wakiwa na safu kali ya ushambuliaji ikiongozwa na Ousmane Dembele. Dembélé amesema Arsenal "wana nguvu kila eneo, na ni hatari kwenye mipira ya ikabu ukizingatia pia Arsenal hawajapoteza mchezo wowote msimu huu wa Champions League.

Arsenal wanatafuta taji lao la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku PSG wakisaka kuwa klabu ya kwanza ya Ufaransa kutwaa kombe hilo mara mbili.